
Umati mkubwa wa watu ulikusanyika kwenye eneo hilo baada ya mlipuko huo ulioacha shimo kubwa barabarani.
Israel ilisema kuwa kuuawa kwa Bwana Jabari, ambaye ni afisa mwandamizi wa ngazi ya juu wa Hamas kuuawa tangu kuvamiwa Gaza miaka minne iliyopita, ni mwanzo wa operesheni mpya dhidi ya wanaharakati hao.

Msemaji wa Jeshi la Wazayuni, Luteni Kanali Avital Leibovitch liongeza kusema kuwa shambulizi hilo ni 'mwanzo wa operesheni kubwa.'
'Lengo la operesheni hii ni kutatiza shughuli za kamandi hiyo na kudhibiti mlolongo wa uongozi wa Hamas na miundombinu yake. Hii ilikuwa operesheni kubwa iliyoshirikisha shirika la usalama la Israel, iliyotekelezwa kwa msingi wa intelejensia kubwa na kutumia uwezo wa hali ya juu,' ilieleza taarifa hiyo ya IDF.
Katika vita ya wiki tatu huko Gaza baina ya Desemba 2008 na Januari 2009, mamia ya watu waliuawa, wengi wao wakiwa raia wa kawaida, na maelfu ya nyumba kuharibiwa vibaya.

Kiongozi wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu iliuhesabu mzingiro huo kuwa wa haramu.
Bwana Jabari alikuwa katika orodha ya juu ya watu wanaotafutwa na Israel na alilaumiwa na Wazayuni hao kwa utekwaji wa askari wa Kiisrael Gilad Shalit mwaka 2006.
Hamas, ambayo siku za karibuni ilianzisha mashambulizi ya roketi kwenda Israel kwa kushirikiana na wanaharakati wengine wa kijeshi, iliripoti kufanyika kwa mashambulizi mengine matatu ya anga dhidi ya Gaza.
0 comments:
Post a Comment