MWILI WA ARAFAT WAANZA KUFUKULIWA KWA UCHUNGUZI

KABUGA KANYEGERI

Kazi ya kufukua kiwiliwili cha Yassir Arafat Kiongozi wa zamani wa Harakati ya Ukombozi wa Palestina PLO ili kuchunguza kifo chake baada ya kufariki dunia miaka minane iliyopita ilianza jana Jumanne.
Ufukuaji huo ambao ulianza jana unatazamiwa kuchukua muda wa siku 15 kutokana na shughuli kuwa ngumu kwa sababu inahitajia kufanywa kwa kutumia mkono. Hayo yamesemwa na wataalamu wa Uswisi na wachunguzi wa Russia.

Mwili wa Yassir Arafat uliamuliwa kufukuliwa baada ya maafisa wa Ufaransa kufungua mashtaka mwaka huu kuhusiana na kifo chake baada ya wanasayansi wa Uswisi kugundua kwenye baadhi ya vitu vyake sampuli za mada nururishi kwa jina la polonium.
Polonium inatajwa kuwa mada yenye sumu ya kiwango cha juu na ambayo mara chache hupatikana nje ya maeneo ya shughuli za kijeshi na kisayansi.

IRIB.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment