CCM imemteua Abdulrahman Kinana kuwa Katibu Mkuu mpya. Uteuzi huo umefanyika leo katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, NEC kwenye mkutano wake wa mjini Dodoma.
Katika uteuzi huo Vuai Ali Vuai ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Zanzibar huku Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara ikichukuliwa na Lameck Madelu Nchemba.
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro amechukua nafasi ya Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa.
Akizungumza katika kikao hicho, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM amewashukuru wajumbe wapya wa Halmashauri Kuu ya Taifa na amewataka kuchapa kazi na kujenga mustakabali mzuri wa Chama.
 |
| Abdulrahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM, Taifa. | | | | |
 |
Mwigulu Nchemba-Naibu Katibu Mkuu (Bara)
| | | |
 |
| Vuai Ali Vuai-Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar) |
 |
| Nape Nnauye, abakia katika Nafasi yake ya Katibu wa Itikadi na Uenezi. |
 |
| Asha-Rose Migiro- Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. |
 |
| Zakia Meghji-Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha. |
 |
| Muhamed Seif Khatib, Katibu wa NEC, Oganaizesheni. |
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment