UTAFITI: ROBO TATU YA NCHI ZA KIAFRIKA NA ZA KIARABU KATIKA MGOGORO WA CHAKULA
Robo tatu ya nchi za Afrika na mataifa kadhaa ya Kiarabu yapo katika hatari kubwa au mgogoro uliokithiri wa chakula, hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya. Katika utafiti uliofanywa katika nchi 197, ambao ulichapishwa na taasisi ya global risk and strategic consulting firm Maplecroft Jumatano ya leo, nchi 59 zipo katika hatari ya upungufu wa chakula. Uchambuzi huo umeongeza kuwa katika nchi kumi na moja zilizo katika "hatari iliyokithiri", tisa zinatoka Afrika. Nyingine mbili ni Haiti na Afghanistan. Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zinashika nafasi ya kwanza, zikifuatiwa na Haiti, Burundi, Chad, Ethiopia, Eritrea, Afghanistan, Comoro, na Sierra Leone, kwa mtiririko huo. "Pamoja na kwamba mgogoro wa chakula haujaibuka bado, kuna uwezekano wa kutokea mapinduzi yanayohusisha chakula katika maeneo yenye mazingira na hali magumu zaidi," Helen Hodge kutoka Maplecroft alisema. Vyanzo vya uhaba wa chakula vinatokana na vita, kupanda kwa bei za nafaka, na uzalishaji kupungua katika nchi za Urusi ya zamani. "Vyanzo vya Vuguvugu katika mataifa ya Kiarabu vinatofautiana na kwa kiasi kikubwa vilitokana na hali ngumu pamoja na hasira ya muda mrefu waliyokuwa nayo wananchi dhidi ya kukithiri kwa rushwa serikalini na ukandamizaji dhidi ya raia na wapinzani wa kisiasa," Maplecroft ilisema na kuongeza, "Sababu hizi zinapochanganywa na uhaba wa chakula uliosababishwa na kupanda bei kimataifa, zinaweza kujenga mazingira ya machafuko ya kijamii na mabadiliko ya serikali." Mabadiliko muhimu yakilinganishwa na viwango vya mwaka jana yalitokea Korea ya Kaskazini (kutoka 19 hadi 35), Misri (kutoka 88 hadi 71) na Syria (kutoka 89 hadi 16).
0 comments:
Post a Comment