TETEMEKO LA ARDHI NCHINI MEXICO

TETEMEKO la ardhi lenye ukubwa wa 6.0 kwa kipimo cha Ritcha limetingisha eneo moja katika Ghuba ya California kutoka pwani ya Mexico. Kwa mujibu wa Shirika la Utafiti wa Kijiolojia la Marekani USGS), tetemeko hio lilitokea jana Jumapili saa 5: 26 Jioni na kitovu chake kilikuwa maili 45 kusini magharibi mwa mji wa Topolobampo, Sinaloa. Hapakuwepo na ripoti za haraka juu ya maafa au hasara iliyotokana na tetemeko hilo. Mnamo tarehe 20 mwezi wa Machi, tetemeko kali lenye ukubwa wa 7.4 kwa kiwango cha Ritcha kilipiga katika eneo la kusini magharibi, jirani na eneo la mapumziko ya kitalii ya Acapulco. Tetemeko hilo liliua watu wawili na kuharibu takriban makazi 13,500. Kwa mujibu wa shirika la Seisimolojia la Mexco, wastani wa matetemeko saba yenye ukubwa wa zaidi ya 3.0, hupiga katika nchi hiyo ya Amerika ya Kaskazini kila siku.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

1 comments:

  1. ni kipi chanzo cha tetemeko la ardhi kitaalamu {kupitia elimu ya muongozo{dini} na elimu ya mazingira}

    ReplyDelete