UCHAGUZI WA VENEZUELA LEO

Leo wapiga kura nchini Venezuela wanaanza kumiminika katika vituo vya kupiga kura kwenda kumchagua rais mpya huku kukiwa na ushindani mkali kati ya wagombea. Mchuano mkali upo kati ya Rais wa sasa Hugo Chavez na mpinzani wake kutoka chama cha Democratic Alliance Unity, Cabriles Enrique. Maoni ya uchunguzi yaliyotolewa kabla ya uchaguzi yanaonesha kuwa Chavez yuko mbele ya mpinzani wake wa mrengo wa kulia kwa pointi tatu. Waangalizi wanaamini kwamba kama Chavezatafanikiwa kushinda atakuwa rais wa kwanza katika historia ya bara la Marekani kufanikiwa katika chaguzi na kura zote maoni alizoshiriki. Jumamosi ya jana Venezuela ilifunga mipaka yake kwa "watu na magari" kama hatua za kiusalama kabla ya uchaguzi wa rais unaofanyika leo Jumapili. Hayo ni kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Ndani Tarek Alaiseme katika mtandao wa Twitter. Alisema kuwa nchi imeamua "kuzuia mipaka kuanzia saa 12:00 Siku ya Jumamosi mpaka saa 5:59 Jumapii usiku." Jeshi litatekeleza hatua hii katika mpaka wa Venezuela na Brazil, Colombia na Guyana. Ni kawaida kwa Venezuela kufunga mipaka yake wakati wa uchaguzi. Kama hatua za kiusalama, pia, raia wamepigwa marufuku kubeba silaha tangu Ijumaa alasiri hadi alasiri ya Jumatatu. Kadhalika wamekatazwa kuuza vinywaji vikali. Polisi wameamriwa kukaa katika kambi zao na zimewekwa chini ya udhibiti wa jeshi. Kwa upande wake, Waziri wa Ulinzi Henry Rangel Silva alitangaza kwenye mtandao wa Twitter "mikusanyiko ya umma ambayo inaweza kuathiri mchakato wa uchaguzi imezuiliwa." Askari wapatao 139,000 wametawanywa katika kuhakikisha kunakuwepo na usalama katika mchakato huo wa uchaguzi wenye mchuano mkali kati ya rais anayemaliza muda wake Rais Hugo Chavez, ambaye uchunguzi wa maoni unaonesha kuwa atapata ushindi, na mpinzani wake Cabriles Enrique Radunsky ambayo alifanikiwa kupunguza pengo kati yake na Chavez mwishoni mwa kampeni zake.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment