AJALI YA NDEGE NCHINI SUDAN YAGHARIMU MAISHA YA WATU

NDEGE ya kijeshi iliyokuwa imebeba watu 20 imeanguka jirani na mji mkuu wa Sudan, Khartoum. Msemaji wa jeshi la Sudan Sawarmi Khaled Saad anasema kuwa rubani aliutarifu uwanja wa ndege kuwa alikuwa na tatizo kwenye moja ya injini za ndege hiyo iliyoanguka magharibi mwa Jebel Aulia. Idadi ya waliokufa bado haijulikani, lakini baadhi ya vyombo vya habari vimesema kuwa redio ya serikali imeripoti kuwa watu wapatao 15 wamefariki katika ajali hiyo. “Kuna watu wamejeruhiwa, lakini bado tunakusanya taarifa kuhusu idadi rasmi” alisema Saad. Ndege hiyo ilikuwa ikitokea Khartoum kuelekea al-Fasher, mji mkuu wa jimbo la kaskazini la Darfur. Mwezi wa Agosti, ajali ya ndege iliyotokea katika jimbo la mpakani magharibi mwa nchi hiyo iligharimu maisha ya watu 32, akiwemo waziri mmoja wa serikali ya Sudan. Jeshi la Sudan limepoteza ndege zake kadhaa katika miaka ya hivi karibuni
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment