HUYU NDIYE WAZIRI MKUU MPYA WA SOMALIA

Rais mpya wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amemteua Abdi Farah Shirdon Saaid kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo. Kuteuliwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu mwenye umri wa miaka 54 ni uamuzi mkubwa wa kwanza kufanywa na utawala nchini Somalia kwa zaidi ya miaka 20. Hatua hii imekuja baada ya wapiganaji wa al-Shabab kuondoka katika ngome yao kubwa ya mwisho katika mji wa Kisimayo, kabla ya majeshi ya Somalia na Kenya kuudhibiti mji huo wenye umuhimu kimkakati. Hassan Sheikh Mohamud, ambaye naye ni mpya katika ulingo wa siasa, aliapishwa kuwa rais wa nchi hiyo mwezi uliopita. Somalia haijawa na serikali imara tangu mwaka 1991, pale wababe wa vita walipomuondosha madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo Mohamed Siad Barre. Taifa hili la pembe ya Afrika ni miongoni mwa nchi zinazotoa idadi kubwa kabisa ya wakimbizi ulimwenguni na ina idadi ya watu wasiokuwa na makazi ndani ya nchi.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment