HIVI NDIVYO HUGO CHAVEZ ALIVYOSHINDA
Rais wa Venezuela Hugo Chavez ameshinda kwa mara ya nne mfululizo katika uchaguzi uliokuwa na upinzani mkali katika nchi hiyo ya Amerika Kusini. Baraza la Taifa la Uchaguzi lilitangaza jana Jumapili kuwa Rais Chavez alishinga kwa kura nyingi, kwa kupata asilimia 54.42 ya kura, ikilinganishwa na asilimia 44.97 ya mgombea wa upinzani Henrique Capriles. Maelfu ya wafuasi wa rais huyo mwenye umri wa miaka 58 walijimwaga mitaani katika mji mkuu Caracas kusherehekea ushindi, mara tu baada ya rais wa baraza la uchaguzi Tibisay Lucena kutangaza matokeo. Lucena pia alisema kuwa katika asilimia 90 ya kura zilizohesabiwa, Chavez alipata kura 7,444,082, huku Capriles akipata kura 6,151,554. Aliongeza kwamba watu waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi wa nchi hiyo ilikuwa 80.94 asilimia ya wapiga kura milioni 19 wenye uhalali wa kupiga kura. Mgombea wa upinzani mwenye umri wa miaka 40, alimpongeza Rais Chavez kwa ushindi alioupata, ambao utamuweka madarakani kwa muda wa miaka sita baada ya kukaa miaka karibu 14 katika ofisi. Wakati akihutubia wafuasi wake mbele ya ikulu ya rais, Rais Chavez aliwashukuru Wavenezuela kwa kuendelea kumuunga mkono na kuuchukulia uchaguzi huo "vita kamili ya kidemokrasia katika nyanja zote." Chavez, ambaye alinusurika mapinduzi ya mwaka 2002 yaliyoratibiwa na Marekani, ni mkosoaji mkubwa wa siasa za Marekani.Ameweza kupata umaarufu miongoni mwa watu wa hali ya chini kutokana na mkakati wake wa kutumia mapato ya mafuta kuboresha sekta za afya na elimu katika nchi hiyo. Rais wa Venezuela pia amefanya kazi kubwa sana katika kutengeneza muungano madhibuti wa mataifa Kilatini. Rais wa Bolivia Evo Morales alimpongeza Rais Chavez kwa kuchaguliwa tena, akieleza kuwa ushindi huo ni ushindi kwa Amerika ya Kusini. "Sio tu ushindi kwa watu wa Venezuela bali pia ni ushindi kwa ndugu zao wa Bolivia na Amerika Kusini yote." Alisema Morales. Rais wa Ecuado Rafael Correa pia alipongeza ushindi wa Chavez wa. "Viva Venezuela, viva kaka mkubwa, viva Mapinduzi ya Bolivia!" alishangilia Rais Correa.
0 comments:
Post a Comment