WAWILI WAJERUHIWA KATIKA MASHAMBULIZI YA NDEGE KASKAZINI MWA UKANDA WA GAZA

Ndege ya kivita ya Israel aina ya F-16
Kwa uchache Wapalestina wawili wamejeruhiwa katika mashambulizi ya ndege za Israel zilizoushambulia ukanda wa Ghaza. hayo ni kwa mujibu wa taarifa za hospitali.
Ndege za kivita za Israel aina ya F-16 zilifanya mashambulizi hayo Ijumaa Usiku, shirika la habari la China Xinhua limeripoti.
Harakati ya Mapambano ya Kipalestina ya Hamas inasema kuwa katika mwezi wa juni Israel ilinzisha mashambulizi 58 ya angani na ardhini dhidi ya eneo la Ukanda wa Ghaza, ambayo yaliua dazeni ya Wapalestina na kuwajeruhi wengine wengi.
Mara kwa mara jeshi la Israel limekuwa likilishambulia kwa mabomu eneo la Ukanda wa Ghaza, likisema kuwa hatua hizo zinachukuliwa kwa malengo ya kujilinda. hata hivyo, nguvu za ziada zimekuwa zikitumika, kukiuka sheria ya kimataifa na mara zote raia wamekuwa wakiuawa au kujeruhiwa.
Gaza imekuwa katika mzingiro tangu mwaka 2007, ambapo hali hiyo imesababisha kuporomoka kwa viwango vya maisha, ukosefu wa ajira na umaskini wa hali ya juu.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment