TETEMEKO KUBWA LAPIGA MASHARIKI MWA UFILIPINO

 


Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.9 limepiga eneo la mashariki mwa Ufilipino na kuchochea onyo la tsunami katika ukanda huo.
Kwa mujibu wa  Shirika la Utafitit wa Jiolojia la Marekani, tetemeko hilo kubwa limetokea leo Ijumaa katika kina cha kilometa 33 (maili 20) kwenye majira ya saa 2: 47 Jioni kwa majira ya eneo hilo (12: 47 GMT) kilomita 139 mashariki mwa mji wa Sulangan.
Onyo la kutokea kwa tsunami limetolewa kwa nchi za Ufilipino, Indonesia, Taiwan na Japan kufuatia tetemeko hilo.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment