WATATU WAKAMATWA GHANA KWA NJAMA YA MAPINDUZI




Maafisa wa usalama nchini Ghana wamewatia mbaroni watu watatu kwa tuhuma za kununua silaha kwa ajili ya njama ya mapinduzi iliyokuwa imepangwa kutekelezwa katika nchi jirani ya Ivory Coast, ambapo wimbi la mashambulizi yamepelekea watu wasiopungua 20 kufariki dunia mwezi uliopita. Serikali ya Ivory Coast imewatupia lawama waitifaki wa Laurent Gbagbo Rais wa zamani wa nchi hiyo, ambao wengi wao hivi sasa wanaishi uhamishoni huko Ghana kuwa ndio wanaochochea machafuko huko Ivory Coast, ambayo yamezusha wasiwasi wa kuibuka tena ghasia nchini humo baada ya kumalizika machafuko baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka uliopita.
Stephen Andoh Kwofie Naibu Kamishna wa polisi wa Ghana amesema kuwa watu hao watatu walikamatwa Ijumaa iliyopita katika mji wa Cape Coast na maafisa polisi wa Ghana waliojifanya wafanya biashara wa silaha.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment