Karibu watu 20 wameuawa na zaidi ya wengine 30 kujeruhiwa kufuatia mapigano yaliyotokea kati ya koo hasimu katikati mwa Somalia.
Mapigano hayo yaliibuka Jumatano asubuhi katika mji wa MararGur wa Galgaduud na kuendelea kwa masaa saba.
Duru zinaarifu kuwa chanzo cha mapigano hayo ni mgogoro wa muda mrefu kuhusu ardhi za malisho na visima vya maji.
Hali ya wasiwasi imetanda katika eneo hilo na wanawake pamoja na watoto wameripotiwa kukimbia huku wapiganaji wa pande hasimu wakijikusanya kwa ajili ya mapigano mengine.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

0 comments:
Post a Comment