Shirika la Kushughulikia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetaka kutolewa msaada wa dola milioni 39 na laki 8 ili kuwasaidia wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walioko nchini humo na katika nchi za Uganda na Rwanda. Mellisa Fleming msemaji wa UNHCR amesema kuwa, msaada huo ni kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wakimbizi laki 4 walioko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wengine laki 5 walioko katika nchi jirani. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kiwango hicho cha misaada kitatumika katika huduma za kijamii na kuimarisha miundombinu kama vile ujenzi, kujenga vituo vya afya, tiba na madarasa, na pia kujenga bwawa na vyanzo 20 vya maji kwa ajili ya wakimbizi.
Flemming aidha amesema, idadi ya wakimbizi nchini Kongo DRC huenda ikaongezeka, iwapo machafuko na miamala mibovu dhidi ya raia itaendelea kushuhudiwa katika mikoa ya mashariki mwa Kongo.

0 comments:
Post a Comment