Mgombe wa kiti cha Urais nchini Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican Mitt Romney anasema kuwa atakuwa na masimamo mkali dhidi ya Urusi iwapo atachaguliwa kuwa rais.
“Chini ya utawala wangu, marafiki wetu wataona utiifu zaidi, na bwana Putin ataona ulaini mdogo na ugumu na umadhubuti zaidi,” alisema Romney, akimkusudia Rais wa Urusi, Vladmir Putin.
Aliyasema hayo wakati akihutubia katika siku ya mwisho ya Mkutano Mkuu wa chama cha Republican, huko Tampa Florida, siku ya alhamisi.
Aidha, Romney alizikosoa sera za Obama za mambo ya nje, akidai kuwa Rais huyo wa Marekani amekuwa laini mno kwa Iran na Urusi.
Gavana huyo wa zamani wa Massachusetts, siku ya alhamisi alikubali rasmi uteuzi wa Chama chake cha Republican kuwa mgombea, na atachuana na Rais Barack Obama katika uchaguzi utakaofanyika Novemba 6, 2012.
Mgombea huyo alisema kuwa utawala wa Obama umewatupa marafiki muhimu wa Marekani, kama vile utawala wa Israel.
Vilevile, Romney alisema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Marekani, ataimarisha jeshi kuwa na nguvu sana, ambalo hakuna nchi itakayothubutu kulijaribu.”
SAB/HSN/AZ

0 comments:
Post a Comment