Mauritania imemkabidhi kwa Serikali ya Libya Mkuu wa upelelezi wa zamani wa Libya, Bwana Abdullah Al-Senussi.
Senussi aliwasili nchini Libya jana Jumatano na amewekwa kizuizini pamoja na maafisa wengine wa utawala wa marehemu Kanali Muammar Gaddafi, akiwemo waziri mkuu wa zamani. Maafisa hao wamefungiwa katika eneo lisilojulikana ndani ya mji mkuu Tripoli, afisa mmoja wa Libya amenukuliwa akisema hivyo.
“Abdullah al-Senussi atashitakiwa kwa haki kabisa kulingana na viwango vya kimataifa vya haki za binaadamu, haki ambazo wananchi wa Libya walikuwa hawazipati”, hayo yalisemwa na Waziri Mkuu wa Mpito wa Libya, Bwana Abdurrahim al-Keib jana Jumatano.
Makabidhiano hayo yalifanyika baada ya kikao cha ngazi za juu kati ya maafisa wa Mauritania na Libya siku ya Jumanne.
Senussi alikamatwa Machi kwa kuingia nchini Mauritana kinyume cha sheria alipowasili katika mji mkuu wa Mauritania Nouakchott, akitokea Casablanca, Morocco.
Vilevile kachero huyo mkuu wa utawala wa Gaddafi, ambaye atashitakiwa na serikali ya Libya kwa makosa mbalimbali dhidi ya binadamu wakati wa mapinduzi ya mwaka jana, anatakiwa pia na Ufaransa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Senussi anatafutwa kwa hati ya kukamatwa ya ICC iliyotolewa mwaka 2011 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni ukandamizaji wa kikatili dhidi ya maandamano maarufu ya mapinduzi yaliyoiangusha serikali ya Gaddafi.
Aidha, anatafutwa pia na mamlaka za Ufaransa baada ya kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha jela kwa kuhusika na tukio la mwaka 1989 la ulipuaji wa ndege ya Kifaransa huko Niger. Shambulio hilo liliyagharimu maisha ya watu 270, wakiwemo raia 54 wa Ufaransa.
Vilevile Senussi amekuwa akihusishwa na tukio la mwaka 1988 la ulipuaji wa ndege ya Pan Am huko Lockerbie, Scotland, ambapo watu 270 waliuawa.
Walibya walianza vuguvugu dhidi ya utawala wa marehemu Kanali Muammar Gaddafi mwezi Februari, mwaka 2011 na kumuua mwezi Agosti 2011. Alitawala Libya kwa zaidi miongo minne.

0 comments:
Post a Comment