HABARI MPYA KUHUSU MAANDAMANO YA PAKISTAN


Mapambano yaliyozuka baina ya waandamanaji na vikosi vya usalama yameacha vifo vya watu 23 na mamia ya majeruhi.
Makabiliano hayo yalizuka katika miji isiyopungua mitano ya Pakistan Ijumaa ya leo, wakati Polisi walipotumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji.

Katika mji mkuu Islamabad, waandamanaji waliandamana kuelekea kwenye ofisi za balozi zainazopatikana katika mji huo, wakitaka kufukuzwa kwa mabalozi wa Marekani na Ufaransa katika nchi hiyo.

Maelfu ya waandamanaji zaidi walielekea kwenye ofisi za wanadiplomasia wa Marekani katika miji ya Lahore na Karachi.

Katika mjia wa kaskazini magharaibi wa Peshawar, waandamanaji walichoma moto kumbi mbili za sinema na kuyashambulia majengo mengine kadhaa.

Kwa zaidi ya wiki moja sasa, ulimwengu wa Kiislamu umekuwa katika ghadhabu kubwa dhidi ya filamu iliyotengenezwa Marekani inayomtusi mtu Mtukufu zaidi katika Uislamu, Mtume Muhammad (s.a.w) na kuutusi Uislamu pia.




Mnamo Septemba 19, gazeti la wiki la nchini Ufaransa la Charlie Hebdo lilichapisha vibonzo vya Mtume Muhammad (s.a.w) katika kampeni ya kumdhihaki pamoja na hujuma dhidi ya Uislamu.


Siku ya Alhamisi, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ilielezea "mshituko" na masikitiko yake dhidi ya vibonzo hivyo, na kuonya kuwa hatua hiyo "inazidisha moto katika machafuko na msukosuko uliotokana na kutolewa kwa filamu inayouadhalilisha Uislamu".


Aidha, katibu Mkuu wa OIC, Ekmeleddin Ihsanoglu, aliitaka jamii ya kimataifa kuchukua "hatua za dhati dhidi ya matamshi na machapisho yenye kuchukiza na yenye kuhamasisha yanayotolewa kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza."

Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment