MPANGO WA DHARURA KONGO DRC

Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) inazindua operesheni ya dharura kuwasaidia watu milioni 1.2 walioathiriwa na vurugu zinazoendelea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
"Ni muhimu tusisahau kuwa mgogoro huu wa mashariki unatokea katika moja ya nchi masikini zaidi duniani, ambapo watu wapatao milioni 5.4 tayari walikuwa wakikabiliwa na njaa na utapia mlo wa kutisha," UPI ilimnukuu mwakilishi wa WFP nchini DRC, Martin Ohlsen siku ya Ijumaa.


“Katima matukio mengi, watu wameyaacha makazi, mashamba na mifugo yao, vitu ambavyo ni chanzo pekee cha mlo na kipato," alisema. "Kwa hiyo, hata kama wamekimbia kilometa 20 kutoka katika vijiji vyao, hawana msaada wowote kwa familia zao."

Shirika hilo la WFP limesema kuwa limeomba dola za kimarekani zipatazo milioni 81 kwa ajili ya kufadhili mpango huo wa dharura.

“Mpango huu mpya, ambao utayalenga majimbo matano, utawapatia watu biskuti za nishati, zikifuatiwa na chakula cha dharura, au katika maeneo ambayo masoko yanafanya kazi, zitatolewa fedha taslimu au vocha zitakazowaruhusu kununua chakula chao wenyewe," ilisema taarifa ya WFP kwa vyombo vya habari.
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment