Moto ukiunguza soko la vifaa vya ujenzi katika viunga vya mji wa Moscow Oktoba 8, 2017. |
Kwa uchache watu 10 wamepoteza maisha baada ya moto
kuunguza kiwanda cha viatu nchini Russia, huku vibarua saba wa Kichina wakiwa
miongoni mwa waliofariki, maafisa wamesema.
Moto huo kwenye kiwanda kidogo katika kijiji cha Chernorechenskiy,
kiasi cha kilometa 50 (maili 30) kusini mwa mji wa Novosibirsk, ulilipuka
takribani saa 3 asubuhi kwa majira ya eneo hilo, vyombo vya habari vimeripoti.
Moshi mweusi uliosababishwa na kuungua kwa vifaa
ulionekana kuzunguka kiwanda hicho ambacho kilikuwa na wafanyakazi 30.
"Watu wa 10 wamekufa kutokana na moto huo ambao
chanzo chake kimebainishwa. Kwa mujibu wa taarifa za awali, hakuna raia wa
Russia miongoni mwa waliofariki dunia," afisa wa serikali katika eneo hilo
ameliambia shirika la habari la TASS.
Ubalozi mdogo wa Gina katika mji wa Ekaterinburg umesema
kuwa raia saba wa Kichina wamepoteza maisha na mmoja kujeruhiwa.
Taarifa nyingine zinasema kuwa raia wa Kyrgyzstan au Tajikistan
ni miongoni mwa waliopoteza maisha.
Mamilioni ya vibarua kutoka mataifa ya iliyokuwa
Muungano wa Kisovieti katika eneo la Asia ya Kati huingia nchini Russia kila
mwaka kufanya kazi zinazowaingizia kipato kikubwa kutokana na ukosefu wa ajira
katika mataifa yao.
0 comments:
Post a Comment