IBRAHIM ABU THURAYYAH: MLEMAVU WA MIGUU ALIYEUAWA NA MDUNGUAJI WA JESHI LA ISRAEL

Abu Thurayyah was demonstrating against the US decision to recognise Jerusalem as Israel's capital when he was killed [Mohammed Salem/Reuters]
Abu Thurayyah aliuawa wakati wa maandamano ya kupinga uamuzi wa Marekani kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.




Siku mbili kabla ya kuuawa, Ibrahim Abu Thurayyah alitoa ujumbe wa video kwa jeshi la Israel.

"Ninatuma ujumbe kwa jeshi la wavamizi wa Kizayuni,” mlemavu huyo wa miguu mwenye umri wa miaka 29 alisema. "Hii ardhi ni ardhi yetu. Hatutakata tamaa. Marekani inapaswa kuondoa tangazo ililolitoa."

Kabla ya kifo chake, Abu Thurayyah ambaye alikuwa akitembelea beskeli ya walemavu, alikuwa alama muhimu katika maandamano mbalimbali kwenye mpaka wa Ukanda wa Gaza na Israel. Katika wiki kadhaa nyuma, yeye na waandamanaji wenzake waliupinga vikali uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa utawala wa Israel. Katika picha mbalimbali, Abu Thurayyah alionekana akikwea nguzo ya umeme na kutungika bendera ya Palestina.

Mnamo Desemba 15, Abu Thurayyah alipigwa risasi kichwani na mdunguaji wa jeshi la utawala wa Israel.

Yaser Sukkar, ni Mpalestina mwingine aliyeuawa siku hiyohiyo wakati wa maandamano kwenye mpaka wa Gaza. Wapalestina wengine wawili waliuawa na jeshi la Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu, na kufanya idadi ya vifo tangu uamuzi huo wa Trump kufikia Wapalestina wanane.


Mapema leo Jumamos, mazishi yamefanyika kwa ajili ya Abu Thurayyah na Wapalestina wengine watatu waliouawa siku moja kabla.

Msemaji wa Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza, Ashraf al-Qidra, katika taarifa yake leo Jumamosi amesema kuwa jeshi la Israel limekuwa likitumia wadunguaji wenye silaha nzito na kurusha mabomu ya machozi dhidi ya waandamanaji.

"Jeshi pia limekuwa likitumia mabomu ya gesi ambayo ubora wake haujulikani, ambayo yamesababisha majeruhi ya mamia ya watu wanaokumbwa na msukosuko, kutapika, kukohoa na mapigo ya moyo yasiyokuwa ya kawaida," alisema.

Aidha, Qidra ametanabahisha kuwa vikosi vya utawala wa Israel vimekuwa vikitumia nguvu kupita kias dhidi ya raia na kuwalenga kwa makusudi watoa huduma za afya, magari ya wagonjwa na waandishi wa habari.

Abu Thurayyah alipoteza miguu yake miwili na figo moja katika shambulizi la anga la Israel mwezi Aprili mwaka 2008, akiwa amekaa na marafiki zake katika kambi ya wakimbizi ya al-Bureij katikati mwa Gaza. Watu saba waliuawa katika shambulizi hilo.


Waombolezaji wakiubeba mwili wa Abu Thurayyah wakati wa mazishi yake mjini Gaza leo Jumamosi.


Alikuwa mtafutaji pekee wa riziki kwa wanafamilia wake 11 ambao ni wazazi wake wawili wagonjwa, dada zake sita na ndugu wa kiume watatu. Abu Thurayyah, ambaye kabla ya kupoteza miguu yake alikuwa mvuvi, alilazimika kutafuta kazi nyingine ili aweze kulipia bili za makazi yao katika kambi hiyo ya wakimbizi.


Alipata kazi ya kuosha magari ambayo ilimpatia kiasi cha 50-70 shekel (dola 14-20) kwa siku. Baadhi ya nyakati pia alikuwa akiuza mboga za majani sokoni ili kukidhi mahitaji ya familia yake.

Miaka kadhaa nyuma katika mahojiano na Shirika la Habari la Shehab, Abu Thurayyah alielezea matumaini na ndoto zake za baadaye.

"Nina matumaini ya kumiliki nyumba siku moja,” alisema. "Ninatumai kuwa watu wa Ulaya na nchi za Kiarabu watanisaidia baada ya kusikiliza kisa changu ili nikapate matibabu ng’ambo na kupata miguu ya bandia."


Imeandaliwa na Mzizizima 24 kwa msaada wa mtandao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment