Bingwa wa uzani wa juu wa WBA, WBO, IBO na IBF kutoka Ukraine Wladimir Klitschko, akiwa amepozi na mikanda yake kwenye medani ya Esprit Arena mjini Duesseldorf, Ujerumani, 21 Julai 2015. |
Bingwa wa zamani wa uzani wa juu duniani, Wladimir
Klitschko, ametangaza rasmi kustaafu mchezo wa masumbwi.
Mwanamasumbwi huyo raia wa Ukraine mwenye umri wa miaka 41
aliyeanza masumbwi ya kulipwa mwaka 1996 baada ya kushinda medali ya dhahabu
katika michezo ya Olympic mjini Atlanta, alitawala medani ya uzani wa juu kwa
muongo mmoja lakini akapoteza pambano lake na Anthony Joshua raia wa Uingereza
mwezi Aprili baada ya kupigwa katika raundi ya 11.
"Kama mwanamasumbwi mzoefu na mkomavu,
nimefanikisha kila kitu nilichokitamani, na sasa ninataka kuanza maisha yangu
mengine baada ya michezo," Klitschko alisema katika taarifa iliyotolewa na
menejimenti yake.
Alisema kuwa kwa wiki kadhaa alitafakari kabla ya
kufanya uamuzi wa kuhakikisha kuwa ameusahau mchezo dhidi ya Joshua kwenye
uwanja wa Wembley.
"Sikudhani kuwa ningekuwa na safari ndefu na yenye
mafanikio katika mchezo kwa kiasi hicho, ninawashukuru nyote kutoka katika kina
cha moyo wangu," aliwaambia mashabiki wake.
Klitscko,aliyefahamika kwa mashabiki kama 'Dr.
Steelhammer,' anatundika daruga kama mmoja wa wanamasumbwi mahiri wa zama zote
baada ya kutawa ubingwa wa uzani wa juu kwa muda wa miaka tisa na nusu.
Bingwa huyo alishinda mikanda kutoka vyama vya masumbwi
vya WBA, WBO, IBF na IBO. Kuanzia mwaka 2008 mpaka 2012 ndugu wa Klitschko, Vitali akiwa bingwa wa WBC, walitawala ubingwa wa dunia kwa wakati mmoja na kushikilia
mikanda yote muhimu ya uzani wa juu duniani.
Safari ya Wladimir Klitschko ilishuhudia akishinda mara 64
katika michezo 69, kati ya hiyo, michezo 54 alinda kwa knockouts. Alishiriki katika
michezo 29 ya ubingwa wa dunia, ambayo ni rekodi ya kipekee katika masumbwi ya
uzani wa juu.
0 comments:
Post a Comment