Taarifa na data mpya za kiutafiti kuhusu anayefikiria na
kuwaza zaidi kuhusu tendo la ndoa kati ya mwanamke na mwanaume, zimeonesha kuwa
wanaume huwaza tendo mara 34 ndani ya saa 24, huku wanawake wakiwaza tendo mara
18.
Utafiti uliochapishwa katika gazeti la Daily Star la
Uingereza, umebaini kuwa wanawake hufikiria tendo kila baada ya dakika 51 kwa
siku, huku suala la tendo likizisumbua akili za wanaume kila baada dakika 28
ambayo ni mara mbili zaidi ya wanawake.
Tofauti ipo wazi, na kwa kuwa data hizi ni kiwango cha
kawaida kilichofanywa kwa kundi kubwa la watu, baadhi ya watu wanaweza kuwaza
tendo kwa kiwango kikubwa zaidi ya hicho kilichotajwa au kwa kiwango kidogo
zaidi. Imebainika kuwa wanawake huwaza tendo mara 18.6 kwa siku yaani mara moja
ndani ya dakika 51 ukiondoa muda ambao wanakuwa wamelala, huku wanaume wakiwaza
tendo mara 34.2 kwa siku ambayo ni sawa na mara moja ndani ya dakika 28.
Utafiti huo umeongeza kuwa wanawake wanafikiria kuhusu
chakula mara 15.3 kwa siku ambayo ni sawa na mara moja kila baada ya dakika 62,
wanawaza kuhusu usingizi mara 13.4 kwa siku ambayo ni sawa na mara moja kila
baada ya dakika 72. Aidha, imeonekana kuwa wanaume hufikiria kuhusu chakula
mara 25.1 kwa siku ambayo ni sawa na mara moja kwa dakika 38, huku wakiwaza
kuhusu usingizi mara 20 kwa siku ambayo ni sawa na mara moja kila baada ya
dakika 33.
Katika utafiti huo ilibainika kuwa hamu ya mwanaume
kutaka tendo ina nguvu zaidi ya ile ya mwanamke na huwa ni ya moja kwa moja na
ya wazi, tofauti na mwanamke ambaye hamu yake inafungamana na mazingira yake.
Pia imebainika kuwa mwanaume huweza kufika kileleni baada ya dakika 4 tu baada
ya kuanza tendo la ndoa, huku mwanamke akihitaji angalau dakika 10 mpaka 11 ili
kufika kileleni.
0 comments:
Post a Comment