CARRICK NAHODHA MPYA WA UNITED

 

Michael Carrick anasema kuwa ni heshima kwake kuteuliwa kuwa nahodha mpya wa Manchester United baada ya Wayne Rooney kwenda Everton.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 35 atavaa kitambaa cha unahodha baada ya miaka 13 ya Rooney katika klabu hiyo ya Old Trafford kufikia kikomo baada ya kurudi kwenye klabu yake ya utotoni wiki hii.

Carrick, aliyewasili klabuni hapo mwaka 2006 akitokea Tottenham, alisaini mkataba mpya wa mwaka mmoja mwezi Mei, na anasisitiza kuwa itakuwa furaha kubwa kwake kuongoza kikosi hicho cha kocha Jose Mourinho msimu ujao.

Aliiambia tovuti ya Man United: "Ni fahari na heshima kubwa kuwa nahodha wa klabu kubwa kama hiyo. Ni mwaka wangu wa 12 sasa na nilikuja hapa nikiwa na umri wa miaka 25. Sikuwahi kuwaza kuwa nitakuwa hapa kwa muda mrefu na kupata mafanikio makubwa kiasi hiki.

"Kuwaongoza wenzangu na kushughulika na vijana, kuwaelekeza kwa namna moja au nyingine, ni kitu kizuri na ni furaha kubwa. Nilikuja kwenye klabu hii kama mchezaji na sasa nimekuwa shabiki mkubwa.

"Nimekuwa nikiipenda klabu hii tangu utotoni na sasa kuwa katika nafasi hii ni kitu maalumu sana kwangu.”

Msimu uliopitia Carrick alicheza mara 38, ikiwa ni pamoja na mara 23 kwenye Ligi Kuu. Lakini hakuanza mchezo wa ligi mpaka mwezi Novemba na alibadilishwa katika fainali za EFL na Ligi ya Europa.

Yawezekana akatakiwa kukubali kupunguziwa majukumu msimu ujao wakati ambapo United wanafanya harakati za kumsajili kiungo mpya kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Duru zinasema kuwa Eric Dier kutoka Tottenham ni chaguo namba moja la Mourinho kisha Nemanja Matic wa Chelsea.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment