Magari yaliyoungua baada ya ajali ya moto katika mji wa Bahawalpur,
nchini Pakistan, Juni 25, 2017.
|
Mafuta yaliyokuwa yakivuja kutoka katika gari la mafuta
lililopinduka yalishika moto katika mji mmoja nchini Pakistan na kuua zaidi ya
watu 120.
Mtandao wa Geo News wa nchini humo umeripoti leo kuwa
tukio hilo lilitokea katika wilaya ya Pul Paka katika mji wa Bahawalpur baada
ya kundi la watu kujikusanya kwa lengo la kuchota mafuta kwenye gari hilo
lililokuwa limepata ajala kwenye barabara kuu.
Mashuhuda wanasema kuwa watu kadhaa walikuwa wakivuta
sigara kwenye eneo hilo, na kwamba moto uliotokana na sigara hizo unaweza kuwa
chanzo cha mlipuko huo.
Duru za uokozi zinasema kuwa waathirika waliungua vibaya
sana kiasi cha kutotambulika na kwamba kipimo cha DNA kingetumika kuwatambua.
Baadhi ya waathirika ni wenyeji wa wilaya hiyo huku
wengine wakiwa ni wapiti njia.
Magari yalishika moto katika tukio hilo ambalo mtandao
huo wa Geo umesema kuwa ulidhibitiwa.
Zaidi ya watu 100 pia wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Jeshi la nchi hiyo lilisema kuwa litatuma helkopta za
kijeshi kuwaokoa majeruhi. Hospitali zimewekwa katika hali ya utayari mkubwa.
Mwaka 2015 watu wasiopungua 62. Wakiwema wanawake na
watoto, walipoteza maisha kusini mwa Pakistan baada ya basi lao kugongana na
gari la mafuta kusababisha moto mkubwa uliowaunguza watu vibaya sana.
0 comments:
Post a Comment