UCHAGUZI WA GAMBIA: YAHYA JAMMEH AKUBALI KUSHINDWA BAADA YA KUTAWALA KWA MIAKA 22

President Yahya Jammeh
Rais Yahya Jammeh



Imeripotiwa kuwa Rais Yahya Jammeh wa Gambia amekubali kushindwa uchaguzi baada ya kuitawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 22.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo, Alieu Momar Njie, alimpongeza Jammeh na kusema:

“Hakika ni jambo la kipekee kwa mtu aliyeitawala nchi hii kwa kipindi kirefu kukubali kushindwa.”

Mkuu huyo wa tume ya uchaguzi amemtangaza mgombea wa upinzani Adama Barrow kuwa mshindi wa uchaguzi wa kiti cha urais kwa mwaka huu wa 2016. Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:

Adama Barrow –  kura 263,515.

Yahya Jammeh –  kura 212,099.


Image result for Adama Barrow
Rais Mteule, Adama Barrow

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment