Waseem Akhtar, mteule wa umeya wa Chama cha Muttahida Qaumi (MQM) akisindikizwa na na polisi baada ya upigaji kura wa kuchagua meya katika Jengo la Manispaa mjini Karachi, nchini Pakistan, Agosti 24, 2016. |
Mji wa Karachi ambao ndio mji mkubwa kabisa nchini
Pakistan wenye zaidi ya wakazi milioni 20, umemchagua meya mpya ambaye yuko
gerezani na anasema kuwa atauongoza mji huo akiwa korokoroni.
Waseem Akhtar, ambaye ni mbunge wa zamani, alichaguliwa
jana Jumatano kuwa meya wa mji huo wakati akiwa katika jela kuu ya Karachi
ambapo ameshikiliwa kwa miezi kadhaa.
“Akhtar alikamatwa mwezi Julai kwa tuhuma za kuwasaidia
wanamgambo na wahalifu kwa kuwapatia hifadhi na matibabu. Pia Akhtar
alishitakiwa kwa tuhuma mbalimbali za kuhamasisha ghasia mwezi Mei mwaka 2007
zilizoutikisa mji wa Karachi. Akikutwa na hatia, atabaki jela kwa miaka kadhaa”,
inasema ripoti ya mtandano wa Quartz.
Akhtar aliteuliwa na Harakati ya Muttahida Qaumi (MQM),
chama cha kisiasa ambacho kimeuongoza mji huo kwa miongo kadhaa. MQM
inajulikana kwa kuendesha tawi la wanamgambo lenye utata. Kukamatwa kwa Akhtar
ni sehemu ya operesheni ya jeshi dhidi ya ufisadi wa kisiasa na ghasi
mbalimbali katika mji huo, kwa mujibu wa Quartz.
Meya huyo mpya ameapa kuuongoza mji huo wenye utajiri
mkubwa zaidi nchini Pakistan akiwa gerezani, akisema kuwa ataomba idhini ya
kuwa na ofisi gerezani na kuweka “kanuni mpya” ili watu waweze kumfikia kwa
urahisi. Ikilazimika atatumia kiunganishi cha video kwa kipindi chote cha miaka
mitano ili kuuongoza mji huo akiwa gerezani.
“Hakuna ukumbi wa mikutano gerezani ambao una ukubwa wa
kutosha kwa mikutano ya manispaa… Maandalizi yanaweza kuwa magumu kwa maafisa
wa jela. Nina shaka kwamba meya mpya atalazimika kumpa mamlaka naibu wake
kuendesha baadhi ya vikao,” afisa mmoja wa serikali ya Pakistan ameliambia
Gazeti la Financial Times.
CHANZO: CCTV Africa
Ungana nasi kupitia WhatsApp: +255 712 566 595
0 comments:
Post a Comment