Michelle Ekure ni binti mrembo wa Kinigeria aliyezaliwa
katika familia ya Bwana Ekure katika Jimbo la Delta nchini Nigeria.
Binti huyu ni mhitimu wa Taaluma za Kimataifa na
Diplomasia katika Chuo Kikuu cha Benin. Katika kukabiliana na ukosefu wa kazi
aliamua kujishughulisha na utengenezaji na ubunifu wa viatu yeye mwenyewe.
Katika mahojiano na Lukmon wa Wazobia Global Times,
Michelle alielezea safari yake ya kuingia kwenye tasnia ya utengenezaji wa
viatu.
Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano hayo:
Lukmon:
Kwa nini uliamua kuingia kwenye fani ya utengenezaji viatu?
Michelle: Nadhani Mungu ndiye
aliyeniongoza, kwa sababu sikuwa na wazo lolote kwamba siku moja nitakuwa
mtengeneza viatu. Nilihitimu masomo ya Chuo Kikuu miaka sita iliyopita,
nikatafuta kazi lakini sikupata. Wakati fulani niliajiriwa kwenye kampuni moja
mjini Lagos, lakini bosi alikuwa na manyanyaso kupita kiasi, hivyo nikaamua
kuondoka.
Na kuhusu nilivyoanza: Kuna kampuni ambayo ninanua viatu
vya wazi mjini Lagos na kuviuza. Wanauza viatu vizuri. Hivyo siku moja niliwaza
iwapo naweza kuwaambia watu hawa wanitengenezee viatu vya wazi (sandals) vyenye
nembo yangu, nikawaeleza wakakubali. Hivyo ndivyo nilivyopata jozi ya kwanza ya
viatu vyangu. Kisha rafiki yangu mmoja alinitambulisha kwa mtu anayetengeneza
viatu. Nilimtazama anavyotengeneza na nilishangazwa sana, nikamuomba
anifundishe, akakubali.
Lukmon:
Mwanzo
mzuri sana.
Michelle:
hmm.
Ahsante.
Lukmon:
Sasa
unawezaje kufanya mauzo na wateja wako ni watu gani?
Michelle:
Wateja
wangu ni wanaume wenye heshima zao, watu kama vile mchekeshaji maarufu wa
Nigeria Alibaba… ninafanya mauzo ya moja kwa moja, lakini ninafanya mauzo mengi
zaidi kupitia mitandano ya kijamii kama vile instagram, facebook na twitter. Ninauza
zaidi ya jozi 50 kwa wiki.
Lukmon:
Ni
mafanikio makubwa! Hiyo ni idadi kubwa. Bila shaka utakuwa mchapa kazi sana. Una
washirika?
Michelle:
Kwa
sasa hapana, labda wakati fulani nitakuwa nao. Lakini nina watu ambao
ninawafundisha.
Lukmon:
Una
wanafunzi wangapi?
Michelle:
Wapo
kama 6 hivi na wengine wanaendelea kuja.
Lukmon:
Kuhusu
mchekeshaji maarufu wa Nigeria, Alibaba. Tumeona picha mbalimbali ukiwa naye. Je,
mna uhusiano au udugu wowote?
Michelle:
Hapana,
hatuna uhusiano. Lakini ni kama baba yangu. Daima anapenda kuona nikifanikiwa.
Lukmon:
Hivyo,
kama si utengenezaji viatu, ungekuwa wafanya kazi gani?
Michelleo:
Labda
ningefanya kazi katika masuala ya kimataifa, kwenye ubalozi au kwenye ofisi ya
Umoja wa Mataifa. Ninapenda kuwa mwanadiplomasia.
Lukmon:
Hmm.
Hilo linaweza kutokea siku moja.
Michelle:
Ni
kweli. (anatabasamu).
Lukmon:
Una
ushauri gani kwa mabinti ambao hawajapata njia ya kutokea?
Michelle:
Daima
huwa nawaambia watu ninaokutana nao na wanaotafuta kitu cha kuanzia kwamba,
chochote unachoweza kukifanya na kikakupatia pesa kifanye, au jifunze kufanya
biashara yoyote.
Lukmon:
Ahsante
kwa kutupa fursa ya kuongea na wewe, tunakushukuru sana.
Michelle:
Karibu
tena Lukmon.
NINI MAONI YAKO? TUPIA MAONI YAKO HAPA CHINI.
Ungana nasi katika WhatsApp: +255 712 566 595
0 comments:
Post a Comment