Jukwaa la Wanahabari wa Kipalestina limeishukia Google
kwa kufuta jina la Palestina kwenye ramani zake na kuweka jina la Israel.
Katika taarifa yake ya jana, jukwaa hilo lilisema kuwa uamuzi
wa Google wa kuiondoa Palestina katika ramani zake ilioufanya tarehe 25 Julai “ni
sehemu ya mpango wa Israel wa kuasisi jina lake kama dola halali kwa vizazi
vijavyo na kuifuta kabisa Palestina.”
“Hatua hiyo inakusudia kupotosha historia, jiografia na
haki ya Wapalestina ya kudai ardhi yao, na ni jaribio haramu la kucheza na
akili za Wapalestina, Waarabu na dunia kwa ujmla.”
Jukwaa hilo limesema kuwa hatua hiyo ni “kinyume na
mapatano na mikataba yote ya kimataifa”, huku likisisitiza kuwa Google
inatakiwa kurudi nyuma kwenye hatua zake hizo.
0 comments:
Post a Comment