Wanausalama na askari wa kikosi cha kuzima moto wakiwa kwenye eneo lililotokea shambulizi la bomu kwenye mji wa Khalis, mashariki mwa Iraq, on Julai 25, 2016. |
Kwa uchache watu 18 wapoteza maisha na wengine 23
kujeruhiwa katika mlipuko mkubwa uliotokea katika mji mmoja kwenye jimbo la
Diyala nchini Iraq karibu na mpaka na Iran.
Duru za usalama kutoka nchini humo zinasema kuwa shambulizi
hilo la bomu limetokea leo asubuhi katika mji wa al-Khalis, kilometa takribani
15 15 (maili 9) kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa jimbo la Baqubah.
Mkuu wa baraza la jimbo, Omar Maan al-Korawi, amesema
kuwa gari lililobeba vilipuzi lililipuka karibu na lango la Idara ya Kilimo
katika mji huo.
Mpaka sasa, hakuna mtu au kundi ambalo limedai kuhusika
na shambulizi hilo.
Tukio hilo linakuja ikiwa ni siku moja tu baada ya
shambulizi la bomu kwenye kizuizi cha usalama katika mji wa Kadhimiyah wenye
wakazi wengi wa Kishia, kaskazini mwa mji mkuu Baghdad kuua raia wasiopungua 10
na polisi wanne.
Afisa mmoja wa polisi alisema kuwa kwa uchache watu 31
walijeruhiwa katika shambulizi hilo.
Takwimu mpya zilizotolewa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa
nchini Iraq zinaonesha kuwa jumla ya Wairaq 662 waliuawa na wengine 1,457 kujeruhiwa
katika vitendo vya kigaidi, ghasia na mgogoro wa kivita katika mwezi wa Juni.
Kwa mujibu wa ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa, idadi ya
raia waliokufa ni 382. Ghasia pia ziligharimu maisha ya askari 280 wa vikosi
vya usalama ndani ya mwezi huo. Sehemu kubwa ya vifo ilitokea mjini Baghdad, ambapo
raia 236 waliuawa.
Maeneo ya kaskazini na magharibi mwa Iraq yamekumbwa na
ghasia tangu kundi la Dola ya Kiislamu kuanza harakati zake nchini humo mwezi
Juni mwaka 2014.
Vikosi vya serikali ya Iraq, vikiungwa mkono na wapiganaji
wa kujitolea, vimekuwa vikijaribu kuwaondosha wanamgambo hao nchini humo.
WhatsApp: +255 712 566 595
0 comments:
Post a Comment