Wananchi wa Mexico wakitazama damu mahala ambapo Meya Domingo Lopez Gonzalez aliuawa katika mji wa San Juan Chamula, jimbo la Chiapas, Julai 23, 2016. |
Mameya wawili wameuawa kwa kupigwa risasi ndani ya siku mbili
katika mtaa mmoja wenye ghasia nyingi za wababe wa madawa ya kulevya nchini
Mexico.
Mamlaka nchini humo zinasema kuwa meya Ambrosio Soto
Duarte kutoka katika mji mmoja maarufu kwa usafirishaji wa madawa ya kulevya
katika jimbo la Guerrero kusini mwa nchi hiyo, alipigwa risasi siku ya Jumamosi
jioni kwa majira ya nchi hiyo.
Imeripotiwa kuwa watu wenye silaha waliweka kizuizi
kwenye njia kuu katika jimbo jirani la Michoacan wakiwa na magari kadhaa na
kulishambulia kwa risasi gari la meya huyo.
Maofisa wawili wa serikali kuu waliokuwa wakimlinda meya
huyo walijeruhiwa katika shambulizi hilo.
Maafisa wanasema kuwa Soto alipokea vitisho kutoka kwa
kundi moja la wauza madawa ya kulevya na alikuwa akilindwa na maafisa wa polisi
kutoka serikali kuu.
Guerrero ni miongoni mwa majimbo hatari na yenye ghasia
nyingi nchini Mexico. Imekuwa sehemu ya matukio mengo ya utekaji na mauaji
yanayohusisha biashara ya madawa ya kulevya.
Mauaji hayo yametokea baada ya meya mmoja na watu wengine
wanne kupigwa risasi na kuuawa katika mji wa San Juan Chamula kwenye jimbo la
Chiapas kusini mwa nchi hiyo siku ya Jumamosi.
Meya huyo alikuwa kwenye mkutano na wananchi ambapo watu
wenye silaha walikuja na kuufyatulia risasi mkutano huo. Makumi ya watu
walijeruhiwa na kupelekwa hospitali.
Maofisa wanasema kuwa watu sita walikamatwa kuhusiana na
shambulizi la Jumapili.
Ambrosio Soto Duarte, meya wa mji mmoja katika jimbo la Guerrero nchini Mexico, aliuawa kwa kupigwa risasi mnamo Julai 23. 2016. (picha ya maktaba) |
Jumla ya mauaji 324, yote yakihusiana na vikundi vya
uhalifu na madawa ya kulevya, yaliripotiwa kutokea katika jimbo hilo ndani ya miezi miwili kati ya Oktoba na
Desemba mwaka jana, kwa mujibu wa takwimu rasmi.
Mexico imekuwa katika ghasia za vita vya madawa ya
kulevya ambavyo vimegharimu maisha ya makumi kwa maelfu ya watu. Kwa uchache
mameya 75 wameuawa nchini humo katika kipindi cha muongo mmoja.
WhatsApp: +255 712 566 595
0 comments:
Post a Comment