Kwa nini matajiri huzidi kuwa matajiri? Mara nyingi sio
kwa sababu ya bahati. Sio kwa sabbau ya familia walizozaliwa. Sio kwa sababu
wameshinda bahati nasibu. Matajiri hufanya mambo tofauti na watu wengine.
Miongoni mwa maswali ambayo watu wengi wamekuwa
wakijiuliza ni pamoja na sababu za pengo la kipato kuendelea kuongezeka. Katika
utafiti wangu, kuna mambo matano ya awali ambayo matajiri hufanya tofauti na
watu wengine. Mambo hayo ni haya yafuatayo:
1. WANATHUBUTU:
Wanajaribu vitu mbalimbali, wakiwa tayari kwa lolote. Wanafanya
uthubutu huo kwa sababu wanajua kwamba kuanguka ni sehemu ya mchakato wa
kugundua kipi hasa kitakachofanikisha kujenga himaya kubwa zaidi ya utajiri
wao.
2. WANAJIWEKEZEA:
Matajiri hawaitazami pesa waliyoitumia katika
kujistawisha kuwa ni gharama, bali huichukulia kama uwekezaji.
Wanaponunua kitabu, wanapomwajiri mkufunzi, wanapojiunga
na makundi ya kunoa bongo zao au kitu kingine kitakachowaongezea maarifa kwa
kulipia, huliona hilo kama uwekezaji.

3. HUSHIRIKIANA
NA WALE WANAOTAKA KUWAIGA
Kuna rafiki yangu mmoja aliniambia: “Ukitaka kuwa
tajiri, suhubiana na matajiri”.
Matajiri wanatambua kuwa wanaweza kukuza utajiri wao kwa
kushirikiana na wale ambao ni matajiri zaidi yao. Binadamu huchukua tabia na
stratejia za wale wanaomzunguka, na matajiri wamejifunza kuitumia fursa hii
kuongeza utajiri wao.
4. MAZOEA
YA ASUBUHI:
Matajiri wana utaratibu maalumu ambao hawauachi asilani,
utaratibu wanaoufanya kila asubuhi.
Mazoea haya ya asubuhi yanaweza kuwa mazoezi, kupitia
malengo yao au kitu chochote kinachowasaidia kuanza siku yao kwa hamasa. Wanaanza
siku yao wakiwa imara na kwa hamasa kubwa, ambapo hufanikisha mambo mengi kabla
ya mchana kuliko yale yanayofanikishwa na watu wengine ndani ya wiki.

5. UPITIAJI
ENDELEVU WA MALENGO YAO:
Matajiri hujiwekea malengo na kisha huendelea kuyapitia
malengo hayo mara kwa mara, kufanya mabadiliko na kuongeza mikakati ya kufikia
malengo hayo. Mchakato huu wa mrejesho wa haraka huwapa fursa ya kufanya
mabadiliko ya haraka kwenye mipango yao ili kuendelea na safari yao kwa kasi
kubwa.
Wakati watu wengi hawazingatii sana kuhusu mustakbali
wao, matajiri hujikumbusha kile siku kuhusu kule wanakoelekea.
WhatsApp: +255 712 566 595
0 comments:
Post a Comment