![]() |
| Moshi ukionekana baada ya shambulizi kubwa kuutikisa mji wa Kabul nchini Afghanistan leo Aprili 19, 2016 |
Watu wengi wameuawa na wengine kujeruhiwa katika mlipuko
uliotokea katikati ya mji wa Kabul, Afghanistan mapema leo asubuhi, Rais Ashraf
Ghani amesema.
Kituo cha televisheni chan Tolo News cha nchini humo kimesema
kuwa kwa uchache watu 28 wameuawa na wengine zaidi ya 200 wamejeruhiwa katika
shambulizi hilo lililoratibiwa.
Shambulizi hilo, lililodaiwa kutekelezwa na wanamgambo
wa Taliban, lililenga ofisi za idara kuu ya usalama ya nchi hiyo.
katika taarifa yake, ikulu ya nchi hiyo imelaani vikali shambulizi
hilo na kusema kuwa watu kadhaa wameuawa au kujeruhiwa.
Msemaji mmoja wa hospitali ya huduma za dharura mjini
humo ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa hospitali yake imepokea
askari 8 wa Kiafghan waliojeruhiwa.
Wanamgambo wa Taliban waliongeza mashambulizi dhidi ya
vikosi vya kigeni na vile vya serikali ya Afghanistan tangu walipotangaza
kuanza mashambulizi waliyoyaita kama “mashambulizi ya machipuo” wiki iliyopita.

0 comments:
Post a Comment