SAUDI ARABIA YAKATA UHUSIANO WA KIDIPLOMASIA NA IRAN




Saudi Arabia imetangaza kuwa inakata uhusiano wa kidiplomasia na Iran kufuatia tukio la ubalozi wake mjini Tehran kushambuliwa jana wakati wa maandamano.

Waziri wa mashauri ya kigeni ya taifa hilo, Adel al-Jubeir, ametoa tangazo hilo huku wizara yake ikisema kuwa inawataka wanadiplomasia wa Iran kuondoka nchini humo ndani ya saa 48.

Aidha, wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia imesema kuwa wafanyakazi wake katika ubalozi wake wameondoka mjini Tehran.

Taarifa zaidi itakujia hapa hapa....



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment