
Kocha wa klabu ya Arsenal, Arsène Wenger, amesema kuwa
anapanda na kushuka ili kukiimarisha kikosi chake katika dirisha la usajili litakalofunguliwa
mwezi Januari.
Meneja huyo wa washika bunduki wa Emirates ana upuungufu
kwenye eneo la kiungo kufuatia kujeruhiwa kwa Francis Coquelin, Santi Cazorla, Jack
Wilshere, Tomas Rosicky na Mikel Arteta.
“Hakika nitafanya kazi kubwa,” amesema Wenger. “Nimeshakuwa
na kazi kubwa na nilisema mwezi mmoja uliopita kuwa tuna upungufu kwenye
mashindano yote tunayokutana nayo, hususani kwenye eneo la kiungo. Naam,
tutafanya kazi kubwa.”
Arsenal imehusishwa na uhamisho wa kiungo wa FC Basel, Mohamed
Elneny, huku Wenger akikiri kuwa Mathieu Debucky anaweza kuondoka Emirates.
“Kwa bahati mbaya hatuwezi kutangaza chochote kwa sasa
kuhusu mchezaji huyu [Elneny] kwa sababu hakuna chochote kilichofikiwa,”
alisema.
“Sio kwamba haiwezekani [kwa Debuchy kuondoka]. Nitafurahi
kama akibaki, lakini tusubiri.”
CHANZO: Arsenal.com
0 comments:
Post a Comment