![]() |
| Hujaji akipata huduma baada ya ajali ya kukanyagana katika eneo la Mina Septemba 24, 2015 |
Kwa uchache mahujaji 717 wamepoteza maisha na wengine wapatao 863 wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyotokana na kukanyagana katika eneo la Mina
nje ya mji wa Makka, vyombo vya habari nchini Saudi Arabia vimeripoti.
Kituo cha televisheni cha al-Ekhbariya kimeripoti maafa
hayo kutokana na taarifa za polisi ya nchi hiyo.
Tukio hilo limetokea katika eneo la Mina wakati mahujaji
wakishiriki katika tukio la kupiga mawe viguzo ambavyo ni alama ya shetani.
![]() |
| Watu wakiwa wamelala chini baada ya mkanyagano wa mahujaji katika eneo la Mina nje ya mji wa Makka, Saudi Arabia Septemba 24, 2015. |
Kiasi cha watu milioni 2 wanashiriki katika ibada ya
Hijja mwaka huu mjini Makka.
Hayo yanatokea baada ya tukio la winchi ya ujenzi
kuanguka katika Msikiti Mkuu wa Makka na kuua zaidi ya watu 100 huku zaidi ya
watu 200 wakijeruhiwa.
Taarifa zaidi zitakujia hapa hapa.


0 comments:
Post a Comment