VIKOSI VYA ISRAEL VYAVAMIA MSIKITI WA AL-AQSA, WAPALESTINA WAJERUHIWA

The picture taken on September 14, 2015 shows Palestinian worshipers after Israeli soldiers closed the entrances at the al-Aqsa Mosque.
Picha ikiwaonesha waumini wa Kipalestina baada ya askari wa Israel kufunga lango la Msikiti wa al-Aqsa leo Septemba 14, 2015.

Zaidi ya askari 200 wa Israel wamevamia katika Msikiti wa al-Aqsa Mashariki wa Jerusalem, na kuwafyatulia Wapalestina risasi za mpira na gesi ya kutoa machozi.

Mkurugenzi wa Msikiti wa al-Aqsa, Sheikh Omar al-Kiswani, amesema kuwa kwa uchache Wapalestina sita, akiwemo mzee mmoja, wamejeruhiwa wakati wa siku ya pili ya uvamizi kwenye msikiti huo.

Wapalestina kadhaa pia wametiwa nguvuni wakati wa shambulizi hili jipya.

Tukio la leo linafuatia uvamizi uliofanyika kwenye msikiti huo siku ya jana.

Jana makabiliano yalizuka baina ya Wapalestina na vikosi vya Israel kwenye uwanja wa msikiti huo baada ya vikosi hivyo kujaribu kuwaondosha waumini wa Kipalestina kwenye msikiti huo. Tukio hilo lilisababisha Wapalestina watatu kujeruhiwa na baadhi ya mali kuharibiwa.

Kiswani amesema kuwa utawala wa Tel Aviv umelidhibiti kwa nguvu eneo hilo takatifu na kuongeza kuwa kwa sasa vikosi vya Israel vinawadhibiti watu wanaongia na kutoka katika eneo hilo.

Mpalestina aliyejeruhiwa baada ya vikosi vya Israel kuvamia katika msikiti wa Al-Aqsa leo Septemba 14, 2015.


Hatua hiyo ya Israel imekosolewa na kupingwa vikali na mamlaka za Palestina, akiwemo Rais Mahmoud Abbas. 

Ghasia hizo mpya zilitokea baada ya kundi la wahamiaji 120 wa Israel na waziri wa kilimo wa utawala huo kuingia katika msikiti huo, jambo lililopelekea vikosi vya Israel kufunga lango la eneo hilo.

Wakati huo huo, Wapalestina wamefanya maandamano kupinga hujuma hizo mpya zinazofanywa na utawala wa Tel Aviv.


Aidha, Wapalestina wanaituhumu Tel Aviv kujaribu kuuyahudisha mji huo.

Wakati huo huo, Jordan pia imeutuhumu utawala wa Israel kwa kujaribu kubadilisha historia ya al-Quds.

Misri nayo imelaani hujuma hizo na kuzielezea kama ushadidishaji wa dhulma dhidi ya maeneo matakatifu ya Waislamu.

Eneo la Msikiti wa al-Aqsa, lililopo katika mji mkongwe wa al-Quds unaokaliwa kwa mabavu na Israel, ni eneo muhimu katika dini ya Kiislamu. Msikiti huo ni wa tatu kwa utukufu baada ya Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Madina nchini Saudi Arabia.




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment