
Manchester United imetangaza kumsajili Anthony Martial kutoka
Monaco.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 mwanzo alihusishwa
na kuhamia Tottenham kabla ya kusaini mkataba mpya pale Stade Louis II lakini
sasa amekuwa mtu wa sita kusajiliwa na Louis van Gaal katika msimu huu wa
majira ya joto kwa ada ya paundi milioni 36 (yuro milioni 50).
Baada ya Robin van Persie kujiunga na Fenerbahce mwezi
Julai na Javier Hernandez anayetarajiwa kuelekea Bayer Leverkusen, usajili wa
straika mpya ilikuwa kipaumbele cha United kabla ya kufungwa kwa dirisha la
usajili.
Kwa sasa Wayne Rooney amekuwa na uchezaji usioridhisha
katika Ligi Kuu tangu kuhamia Old Trafford mwaka 2004, huku akiwa hajafunga
hata bao moja ndani ya michezo 10, tofauti na msimu uliopita ambapo alifanya
vyema.
Martial amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu sana
katika Ligi ya Ufaransa na inaripotiwa kuwa bosi wa Monaco Leonardo Jardim alikuwa
ametishia kuondoka iwapo angeuzwa kwa United.
0 comments:
Post a Comment