Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani, Mohammed Morsi,
amesema kuwa lilifanywa jaribio la kumlisha sumu gerezani anakoshikiliwa.
Mapema jana, Morsi alisema kuwa alikataa kula chakula
cha magereza alichopewa tarehe 21 na 22 Julai kwa hofu ya kulishwa sumu.
“Kama ningekula, jinai ingetokea,” alisema wakati vikao
vya mahakama vilivyoanza siku hiyo katika mashitaka yanayomkubali ambapo
anashitakiwa kuvujisha siri za usalama wa taifa.
Morsi alisema kuwa kwa uchache matukio matano yalitokea
na yangehatarisha maisha yake iwapo yangefanikiwa.
Aidha, aliitaka mahakama impatie uwezo wa kuhudumiwa na
madaktari wake kwa kuwa anasumbuliwa na tatizo la sukari.
Morsi alikuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia
nchini Misri, na alipinduliwa na aliyekuwa mkuu wa jeshi la nchi hiyo Abdul-Fattah
Al-Sisi Julai 2013. Al-Sisi ndiye rais wa sasa wa Misri.
Mwezi jana, mahakama ilimhukumu Mursi adhabu ya kifo kwa
tuhuma za kuvujisha taarifa za usalama na kusaidia watuhumiwa kutoroka jela. Mursi
na wafuasi wake wamekataa tuhuma hizo na kusema kuwa zimechochewa kisiasa.
Tangu kupinduliwa kwa Mursi, Misri imeshuhudia ghasia
ambazo zilisababisha watu wengi kupoteza maisha.
0 comments:
Post a Comment