![]() |
| Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Senegal, El Hadji Diouf akiwa dimbani. |
Umaarufu wa El Hadji Diouf katika soka na mikiki yake
dimbani vinajulikana ulimwenguni, lakini baada ya heshima aliyoitengeneza
katika michuano ya Kombe la Dunia na Ligi Kuu ya Uingereza, mkongwe huyo anasaka
mafanikio ya kisiasa katika nchi yake ya Senegal.
Straika huyo mwenye umri wa miaka 34 aliyetengeneza jina
lake katika kikosi cha Senegal kilichowaadhiri mabingwa watetezi wa Kombe la
Dunia, Ufaransa, katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo mwaka 2002 nchini
Korea Kusini, anakaribia kuachana na soka akiwa na kilabu ya Sabah FC inayocheza
daraja la pili nchini Malaysia.
Mafanikio yake katika mchezo wa soka yalimpeleka katika
klabu za Sochaux, Rennes na Lens za Ufaransa, kabla ya kuchukuliwa na klabu za
Uingereza na Scotland kama vile Liverpool, Bolton, Sunderland, Blackburn,
Glasgow Rangers, Doncaster Rovers na Leeds United.
Katika tasnia ya soka hakuna anayebisha kuwa ni mchezaji
mzuri na daima hufurahia kuongea na mashabiki wake na wanahabari.
Lakini Diouf pia amekuwa mtu mwenye milipuko ya hasira. Matukio
kadhaa ya kuwatemea mate wachezaji wa timu pinzani na mashabiki yaliweka wingu
katika mafanikio yake katika soka.
Katika mahojiano ya hivi karibu na shirika la habari la
AFP mjini Kuala Lumpur, Diouf alisema kuwa hatua ya timu yake ya taifa kufikia
robo fainali katika mashindano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2002 ndio kiwango cha
juu alichofikia katika maisha yake ya soka.

0 comments:
Post a Comment