![]() |
| Mchungaji Mtikila |
KATIKA UCHAGUZI MKUU
HUU
TUSIRUHUSU MAFISADI
WALICHEZEE TAIFA
Edward Lowasa ni
balaa kwa Taifa!
Democratic Party
(DP) inatarajia kufikisha Mahakamani chama cha
CCM pamoja na
wanachama wake sita, Edward Lowasa na wengine,
kwa mujibu wa Ibara
ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, kwa kosa
kubwa sana la
kuvunja Katiba na Sheria za Nchi kwa kuanza kampeni
ya Uchaguzi kabla ya
wakati unaopasa kwa mujibu wa Sheria.
1 Tunao ushahidi
mzito unaothibitisha kwamba Edward Lowasa na
wenzake walianza
kampeni ya urais ndani ya chama chao kabla ya
wakati, na kwamba
chama chao kiliwapa adhabu ya kutofanya siasa
kwa miezi 12. Lakini
safari hii Lowasa ameanza kampeni ya urais
Arusha kwa mkutano
mkubwa sana wa hadhara wa kampeni haramu
na kumwaga rushwa ya
kutisha!
2 Kama ni wadhamini
alipaswa kuwapata katika ofisi za chama chake,
katika mikoa nane
(8) tu Tanganyika na mikoa miwili tu Unguja na
Pemba, wadhamini 45
tu katika kila mkoa. Lakini Edward Lowasa
amefanya mikutano
nchi nzima, ya kuwaahidi maelfu ya wananchi
katika kila mkutano
wa hadhara, mambo atakayofanya kama wakimpa
kura zao awe Rais! Hii
ndiyo kampeni halisi, ambayo ni ukiukaji wa
Katiba na Sheria za
Nchi! Uchaguzi Mkuu unaendeshwa na Sheria, hivyo
ni lazima Sheria
ichukue mkondo wake dhidi yake kwa kuivunja.
3 Edward Lowasa amevunja
Katiba ya Nchi na Sheria ya kiwango cha
fedha
kinachoruhusiwa kutumika katika shughuli halali za Uchaguzi,
kiasi kwamba CCM na
Taasisi zote za uchunguzi wa kifedha nchini,
upelelezi wa Jinai
na Usalama wa Taifa ni mlazima wanayo kazi muhimu
sana ya kupata
ukweli kuhusu haya mabilioni ya fedha yanayomwagwa
nchini na fisadi
Edward Lowasa, ameyapata wapi na kwa namna gani,
kumehusika ‘’Money
laundering’ au la, kama mapato ya mapesa hayo
yote ni halali, na
kama mapato hayo yote yalilipiwa kodi inayopasa kwa
ajili ya Taifa.
Ni marufuku kabisa
tena ni makufuru Edward Lowasa kuruhusiwa
kugombea urais, kwa
sababu amevunja Katiba ya Nchi na Sheria na
Kanuni za Uchaguzi. Sifa
mojawapo ya kustahili kugombea uongozi wa
nchi yoyote ni
maadili mema na uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na
taratibu za Utawala wa Sheria
4 Edward Lowasa, kwa
kujimilikisha maeneo nchi nzima kwa kutumia
kifisadi Uwaziri
wake wa Ardhi, ameliweka Taifa katika hatari kubwa ya
mmwagiko wa damu
baina ya wakulima na wafugaji, baada ya kueneza
nchi nzima makundi
ya ng’ombe wake, na kusababisha mapigano
makali ya mara kwa
mara kila mahali nchini kati ya wafugaji wake na
wakulima. Kwa sababu
ya uovu huu hata katika kampeni yake haramu
Lowasa ameshindwa
kusema lolote juu ya kilimo, ingawa ndio uti wa
mgongo wa uchumi wa
nchi yetu na ndiyo shughuli inayotunza uhai wa
asilimia 95 ya
wananchi!
Kwa kuwaingilia
wakulima katika ardhi yao, kuwaua ovyo, kuwaonea
kiasi cha kufisha
matumaini yao katika kilimo, kumeifanya kauli mbiu
ya “Kilimo kwanza” kuwa
porojo tu ya kisanii!
5 Edward Lowasa ni
mwiko kabisa kupewa kugombea urais, kwa
sababu siyo tu
aliutumia kifisadi Uwaziri wa Ardhi akajitajirisha na
kujipatia maeneo
makubwa ya ardhi nchini kote, bali alitumia kifisadi
zaidi uwaziri wa
nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, katika uagizaji wa
mashangingi ya
Wabunge, mawaziri, wakuu wa Mikoa na Wilaya.
6 Edward Lowasa alikemewa
mnamo mwaka 1995 na Mwalimu Nyerere
anayeenziwa na CCM
lama “Baba” yao, alipotaka kugombea urais, kwa
sababu alikuwa fisadi
papa, wala hakuweza kujitetea kwavile utapeli
wote
aliojitajirishia ulikuwa mezani. Leo baada ya mabiashara haramu
mengi na kulipora
sana Taifa kukiwa ni pamoja na utapeli wa “kununua
mvua Thailand” na
kuliibia Taifa mabilioni ya fedha kwa kutumia
kampuni hewa ya RICHMOND,
huyu ni fisadi-nyangumi. Ni mlemavu
wa rushwa tu wa
kununuliwa na mapesa machafu anayomwaga Lowasa,
anayeweza kumruhusu
fisadi Edweard Lowasa agombee urais.
Sifa za mtu wa
kukugombea Urais zimeelezwa bayana na Mwenyezi
Mungu katika Kumbukumbu
la Torati 17:15-20, ambazo Edward
Lowasa hana hata
mojawapo! Lowasa awali alikemewa na Mwalimu
Nyerere ambaye CCM
wanamuenzi kama “Baba” yao, kuwa hafai kabisa
kuwania urais, kwa
sababu alikuwa fisadi papa, kama alivyomtangaza
hata Reginald Mengi
pale alipolazimika kujiuzulu Uwaziri Mkuu kwa ajili
ya wizi kwa kampuni
hewa ya Richmond, lakini leo akiwa fisadi la
kutisha zaidi kuliko
papa eti anataka urais!
Si ajabu kwamba
magabacholi yalioipora vibaya sana Nchi hii kama Sigh
Setti na hata Nazir Karamagi wote wamo
katika genge la Edward
Lowasa! Si ajabu
hata fisadi Reginald Mengi leo kuungana na fisadi
Lowasa yakizingatiwa
machafu yake yeye mwenyewe, na kuhusika kwa
Mengi na mauaji ya
Chacha Wangwe, pamoja na mpango wa Chadema
wa kumwua Mchungaji
Mtikila, waraka feki wa kujaribu kuupotosha
ukweli ukatangazwa
kwa ITV yake.
Katika uwaziri wake
katika ofisi ya Waziri Mkuu, na katika Uwaziri wake
wa Ardhi na Uwaziri
Mkuu, Lowasa alifanya ufisadi ambao katika nchi
kama China zenye
uchungu na maslahi ya mataifa yao angekuwa wa
kupigwa risasi
hadharani, lakini katika nchi yetu anatafuta urais!
7. Edward Lowasa
AFYA yake imempiga marufuku kugombea Urais!
Kwa ajili ya kila
ajira duniasni kote, moja ya mashart makuu ni lazima
mwombaji awe na afya
iliyo bora, ndiyo sababu ni lazima ajira ya kila
mwombaji itegemee
taarifa ya kitaalamu ya madaktari, inayothibitisha
kwamba hana dosari
kiafya. Sharti hili ni la lazima kwa sababu:
a. Majukumu yote
atakayopewa mwajiriwa atayatekeleza kikamilifu
kwa kutumia viungo
vya mwili wake, kwahiyo viungo vyake vyote
ni lazima viwe
katika hali iliyo imara kwa ajili ya kazi.
b. Hata kama kwa
uthibitisho wa kitaalamu wa madaktari mwajiriwa
anazo akili nzuri
kichwani mwake, akiwa na hitilafu katika viungo
vingine vya mwili
wake huathiri afya ya akili zake na uwezo wa
utendaji wa akili
zake.
c. Kazi ya Rais ni
ngumu sana, kwa sababu ni pamoja na kusimamia
shughuli zote za
maendeleo ya nchi nzima, na matatizo yote
yanayowatokea
wananchi wote kila walipo, na kusimamia
utekelezaji wa
majukumu yote ya watendaji wote katika Taifa,
hivyo kwamba maamuzi
sahihi yanatokana na afya bora yenye
kuhakikisha uwezo
unaopasa wa kiakili wakati wote
d. Hitilafu katika
afya hudhoofisha uwezo wa kifikira na kusababisha
maamuzi mabovu,
ambayo huleta athari mbaya sana kwa Taifa. Na
udhaifu huo huathiri
mpaka maadili na hata uzalendo wa huyo
kiongozi mdhaifu.
Kwa mfano akipatikana Rais anayeishi kwa
matumaini, kwa hofu
ya kupoteza uhai kabla hajaweka sawa
mambo yake na ya
familia na jamii yake atatumikia maslahi yake
zaidi kuliko Taifa,
tatizo hilo la afya likawa limelikosesha Taifa
kipaumbele, na kuliangamiza kimaendeleo!
e. Wanaowania
kugombea urais ni lazima wachunguzwe kwa makini
sana afya zao, kwa
sababu kukifanyika makosa akatawazwa
mwenye hitilafu za
kiafya, atakwenda kuwa mzigo mzito sana kwa
Taifa, hususan
ugharamiaji wa utunzaji wa uhai wake ndani na nje
ya nchi, kukosekana
na umakini anaopasa kuwa nao kwa ajili ya
dhamana kubwa
aliyopewa n.k.
Kutokana na AFYA yake
kuwa dhaifu sana hata kwa kumwona kwa
macho tu, kabla ya
uchunguzi wa kitaalamu ni kwamba Edward Lowasa
hawezi kabisa
kugombea Urais. Kwani amekosa sifa muhimu sana ya
afya bora, ambayo ni
ya lazima kwa mtu yeyote anayestahili kupewa
dhamana kubwa sana
ya kuliongoza Taifa. Pengine hata kugombea urais
kwenyewe anatafuta
kutokana na hitilafu ya kiafya, iliyosababisha
udhaifu katika
kufanya maamuzi, hivyo amejikuta kwa bahati mbaya
anagombea
asichokiweza kabisa.
Ni lazima wagombea
wote wa Urais, wa Ubunge na hata wa Udiwani
wachunguzwe kwa
makini afya zao kabla ya kupewa kugombea, na hata
kuchunguzwa tena
katikati ya muhula wa utumishi wao, kama kweli
tunalithamini na
kuliheshimu Taifa.
Sifa za urais ni wito
au uhanga kwa ajili ya Nchi ambao ni zaidi ya
maadili ya
kizalendo, maono, vipawa na AFYA BORA. Ni dhana potofu
sana kwamba sifa ya
urais ni kushabikiwa na umati wa watu! Kwa
sababu wengi hufuata
mapesa na husombwa hata na magari ili umati
wa kishabiki tu
upatikane. Lakini kumpenda mtu huwa lazima kuwe na
sababu, wakati
ushabiki ni pepo mchafu au ‘psychological deficiency’.
CHANZO: http://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania/880358-waraka-wa-mchungaji-mtikila-kwa-edward-lowassa.html

0 comments:
Post a Comment