![]() |
| Watoto waliokimbia machafuko ya Burundi wakisubiri kusajiliwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu Kigoma, Juni 11, 2015. |
Umoja wa Mataifa umesema kuwa watu wapatao 10,000
wameikimbia Burundi mwishoni mwa juma lililopita kabla ya mamlaka za nchi hiyo
kufunga mipaka kabla ya chaguzi zenye utata za bunge na madiwani.
Shirika la Umoja huo linaloshughulikia wakimbizi
limetangaza kuwa jumla ya watu 144,000 wameshaikimbia nchi hiyo tangu kuzuka
kwa ghasia mapema mwezi Aprili mwaka huu.
Msemaji wa shirika hilo Bi Melissa Fleming, amesema kuwa
zaidi ya Warundi 6,000 wakimbilia Tanzania ndani ya kipindi cha siku mbili
pekee. Wengine 4,000 wamekimbilia katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,
Rwanda, na Uganda.
Kwa mujibu wa takwimu za shirika hili, jumla ya
wakimbizi 66,600 wapo nchini Tanzania, 56,500 wapo Rwanda, 11,500 wapo Jamhuri
ya Kidemkrasia ya Congo na 9,000 wapo nchini Uganda.
![]() |
| Wananchi wa Burundi wakiwa katika kituo cha kupiga kura katika uchaguzi wa Wabunge uliofanyika Juni 29, 2015 mjini Bujumbura. |
Mnamo Juni 27, spika wa bunge hilo Pierre Ntavyohanyuma alikimbilia
nchini Ubelgiji.
Uchaguzi wa Juni 29 umefanyika kabla ya uchaguzi wa
urais wenye utata ambao umepangwa kufanyika Julai 17, licha ya wito wa Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kutaka uahirishwe.
Burundi ilianza kushuhudia ghasia za kisiasa mwezi
Aprili baada ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza uamuzi wake wa kugombea muhula
wa tatu.
![]() |
| Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza akihutubia wananchi katika mojawapo ya kampeni za uchaguzi. |
Wapinzani nchini humo wanadai kuwa jaribio la Rais huyo
ni kinyume cha mkataba wa amani wa mwaka 2000 na pia ni kinyume na katiba,
ambapo rais anaweza kuongoza mihula miwili tu.
Ghasia nchini humo zimeshagharimu maisha ya zaidi ya
watu 70 na kuwajeruhi wengine wapatao 500.



0 comments:
Post a Comment