Brela yatoa siku 90 kwa kampuni kuwasilisha hesabu

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), Frank Kanyusi akisisitiza jambo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu kampuni kutakiwa kuwasilisha marejesho ya mwaka yakiambatana na hesabu zilizokaguliwa  kila mwaka. (Na Mpiga Picha Wetu) 

Dar es Salaam. Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela), umetoa siku 90 kwa wamiliki wa kampuni kuwasilisha taarifa zao za mwaka za hesabu zilizokaguliwa vinginevyo zitafutwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Brela, Frank Kanyusi alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa mjini hapa kuwa baada ya muda huo, wamiliki na wakurugenzi wa kampuni hizo watafikishwa mahakamani kwa kosa la kutotoa taarifa za kampuni zao kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni.
“Agizo hili la siku 90 sawa na miezi mitatu, linaanza Oktoba 6, 2014 na litafikia kikomo January 5, 2015,” alisema.
Aidha, matawi ya kampuni za kigeni zilizoandikishwa nchini pia zinapaswa kuwasilisha hesabu zake kila mwaka chini ya kifungu namba 438 kifungu kidogo cha kwanza cha Sheria hiyo.
“Kosa la kutotii sheria hizi adhabu yake ni kufutwa kwa kampuni na wamiliki na wakurugenzi wake kufikishwa mahakamani,” alisema.
Alisema Tanzania ina kampuni 120,000 ambazo zimesajiliwa kisheria, kati yake, kampuni 20,000 tu ndizo zinazowasilisha taarifa zake za kila mwaka.
Alisema hali hiyo siyo nzuri, hivyo Serikali imeamua kulivalia njuga suala hilo ili kuhakikisha kila kampuni inatoa taarifa za kila mwaka za hesabu yaliyokaguliwa na mhasibu anayetambulika kisheria.
“Tunahitaji watu watii sheria bila shuruti na kwa kufanya hivyo, inajenga uhusiano mwema kati ya kampuni na wakala,” alisema.
i vyema jamii na wamiliki wa kampuni hapa nchini wakaona jambo hilo la kisheria na kulizingatia kwa kuwa kufanya hivyo ni kuendelea kuijenga Tanzania.
Alisema sababu kubwa ya kuwa na idadi ndogo ya kampuni zinazowasilisha taarifa za kila mwaka na mahesabu ni kutokana na kampuni nyingi kuendeshwa kifamilia bila ya kuwa na wanasheria wa kampuni.
CHANZO : MWANANCHI
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment