Miili ya watu 12 imeopolewa baada ya kivuko kilichokuwa
na abiria kupinduka na kuzama nchini Bangladesh ya kupigwa na dhoruba kali.
Maafisa wanasema kuwa kivuko hicho kilikuwa kimeondoka
katika kituo kikuu cha Dhaka na kilizama saa kadhaa baada ya kuanza safari
yake.
Baadhi ya abiria waliogelea mpaka nchi kavu huku wengine
wakiwa hawajulikani waliko. Wengine kadhaa waliokuwa wakielea katika mto Meghna
waliokolewa na waokoaji.
Polisi wanasema wanawake na watoto ni miongoni mwa waliokufa.
Idadi ya vifo inaweza kupngezeka kwa kuwa kazi ya
uokoaji inaendelea na kuna uwezekano wa kuopoa miili mingi zaidi.
Matukio ya ajali za vivuko yamekuwa yakiikumba Bangladesh
kwa sababu ya msongamano wa abiria na mfumo mbovu wa usimamizi wa huduma hiyo.
0 comments:
Post a Comment