Jaji mmoja wa mahakama nchini Sudan amemhukumu kunyongwa
hadi kufa mwanamke mmoja wa Kikristo kwa kubadili dini yake.
Kesi hiyo iliyokuwa ikilalamikiwa na balozi za nchi za
Magharibi ambazo zilitaka kutolewa kwa fidia badala ya adhabu hiyo, na ambayo
ni ya kwanza kusikilizwa nchini humo, ilimhusisha mwanamke aitwaye Mariam Yahia
Ibrahim Ishag.
"Tulikupatia siku tatu kutubu lakini ulikataa
kurejea katika Uislamu,” Jaji Abbas Mohammed Al-Khalifa alimwambia mwanamke
huyo ambaye pamoja na adhabu hiyo alihukumiwa kupigwa viboko 100 kwa kosa la
uzunifu.
"Ninakuhukumu kunyongwa hadi kufa."
Wanaharakati nchini humo wanadai kuwa Mariam mwenye umri
wa miaka 27 ni mja mzito na kwamba hakuonesha mshtuko wowote wakati hukumu hiyo
ikitolewa katika mahakama katika wilaya ya Haj Yousef mjini Khartoum.
Katika utetezi wake, Mariam alidai kuwa yeye ni Mkristo
na hajawahi kubadili au kuikana dini yake.
Akizungumza na shirika la habari la AFP, Waziri wa
Habari wa nchi hiyo, Ahmed Bilal Osman, alisema: “Sio Sudan pekee. Nchini Saudi
Arabia na katika nchi zote za Kiislamu Muislamu haruhusiwi kubadili dini yake.”
Serikali ya Sudan ilianza kutumia Sheria za Kiislamu
mwaka 1983 lakini ni nadra sana kutumika kwa adhabu kubwa zaidi ya viboko.
Baada ya hukumu hiyo makundi yanayopinga na yale yanayotetea
adhabu hiyo yalifanya maandamano, lakini hapakuripotiwa ghasia zozote.
CHANZO: Aljazeera
0 comments:
Post a Comment