Na Magreth Kinabo Maelezo
Rais Jakaya Kikwete leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vya uzazi vya wakinamama na watoto ifikapo mwaka 2015 utakofanyika kwenye ukumbi wa mkutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.
Hayo halisemwa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga,kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk,Neema Rusibamayila wakati akizungumza na waandishi wa habari katika semina ya wakuu wa mikoa na waganga wakuu wa mikoa kuhusu kuboresha afya ya uzazi na watoto.
Aidha Dk. Neema alisema uzinduzi huo utaenda sambamba na uzinduzi wa kadi ya ufuatiliaji(scorecard).
“Lengo la semina hii ni kuwatambulisha juu ya mpago huu ili kila Mkuu wa mkoa kutathimini maeneo yapi yamefanyiwa vizuri na wapi kuhahitajika msisitizo,” alisema.
Alisema katika semina hiyo viongozi hao wamepata uzoefu wa wa mkakati wa mkoa Singida na Mara ili kuongeza kasi hiyo kwa siku 500 zilizobakia.
Akizungumzia kuhusu upunguzaji wa vifo vya watoto, kwa mujibu wa tathimini ya Umoja wa Mataifa UN Tanzania imefikia lengo la milinea yaani vifo 54 kwa kila watoto wanaozaliwa 1000, hata hivyo alisema bado jitihada zinahitajika kupunguza zaidi.
Alisema vifo vya wakina mama kwa sasa ni 454 kwa vizazi hai 100,000
Kwa upande wake, Dk. Ahmad Makuwani kutoka wizara hiyo alisema wakuu wa mikoa na wilaya na timu zao wanawajibu wa kuhakikisha wanapunguza vifo vya uzazi na watoto.
“ Wakuu wa mikoa na wilaya mna kazi kubwa ya kuulizia vifo vimetoa kwa sababu gani mkifanya hivyo mtasaidia kupunguza vifo hivo,” alisema Dk. Makuwani.
Dk . Makuwani alisema lengo la milinea la kupunguza vifo kwa wakina mama ifikapo mwaka 2015 ni 195 kwa vizazi 100,000.
Akizungumzia kuhusu uzoefu wa mkoa wa Singida Mganga Mkuu wa mkoa huo,Dk. Doroth Gwajima alisema ushirikiano wa viongozi ,kuzingatia maadili, nidhamu na kila mtu kuwajibika katika nafasi yake itasaidia kupunguza vifo hivyo.
Mikoa inayoongoza kuwepo kwa vifo vya wakina mama ni ya Kanda ya Mashariki na Kanda ya Ziwa kwa sababu ya mila na desturi na upatikananji wa huduma karibu na watu.
0 comments:
Post a Comment