![]() |
Waziri wa Michezo wa Mauritania Fatma Fal Bent Assouina
Assouina.
|
Waziri mpya wa michezo nchini Mauritania amedai kuwa
hajawahi kutazama mechi yoyote ya michezo na havielewi vifaa vya michezo
muhimu, amenukuliwa na tovuti ya habari ya al Quds leo.
“Ninalazimika kutazama mechi hali ya kuwa sikuwahi
kutazama mchezo wowote katika maisha yangu yote,” Fatma Fal Bent Assouina
Assouina alimwambia mmoja wa mashabiki wake aliyekwenda kumpongeza baada ya
kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Assouina, ambayeni mwanamke wa nne kushika wadhifa huo,
amemrithi Lalat Bint Asharif, ambaye alishika nafasi hiyo kwa kipindi
kisichozidi miezi 8.
Sekta ya michezo nchini Mauritania imekuwa ikikabiliwa
na changamoto nyingi kutokana na ukosefu wa ustadi wa mawaziri mbalimbali wanaoteuliwa
kwenye sekta hiyo.

0 comments:
Post a Comment