![]() |
| Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria, Lakhdar Brahimi, akizungumza na waandishi wa habari juu ya mazungumzo ya amani ya Syria kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva Februari 13, 2014. |
Awamu ya pili ya mazungumzo ya kusaka amani yaliyokuwa
yakifanyika mjini Geneva baina ya serikali ya Syria na wapinzani yamemalizika
bila kupatikana matokeo ya moja kwa moja.
Hayo yamesemwa na msuluhishi wa kimataifa kwenye mgogoro
huo, Lakhdar Brahimi.
Akizungumza na waandishi wa habari juu ya mazungumzo
hayo, Bwana Brahimi alisema:
"Ninafikiri ni bora kwa kila upande kwenda
kutafakari juu ya wajibu wao, na kujua iwapo wanataka mchakato huu uendelee au
la.”
Naye mjumbe wa upinzani, Ahmad Jakal, amesema kuwa
mwisho wa kikao hicho hawakuafikiana juu ya tarehe ya kuendelea na awamu ya
tatu ya mazungumzo hayo:
"Kilikuwa kikao cha muda mfupi na kizito,
kilichotawaliwa na tofauti kuhusu jinsi ya kushughulikia masuala la ghasia na
serikali ya mpito. Brahimi hakupanga tarehe maalumu kwa ajili ya awamu ya tatu
lakini aliweka wazi kuwa anatarajia kutakuwa na awamu nyingine ya mazungumzo,”
alisema.
Mgogoro wa Syria umegharimu maisha ya watu zaidi ya 100,000
tangu Machi 2011.

0 comments:
Post a Comment