
Masanja Mkandamizaji si jina geni masikioni mwa watu
wengi kutokana na uwezo wake wa
kuwavunja mbavu watazamaji pale anapoonekana katika runinga na Kundi la
Orijino Komedi.
Licha ya kufika hapo alipo sasa, anakiri wazi kuwa
amepitia katika maisha magumu hususani wakati alipoamua kuanza maisha binafsi
ya kujitegemea baada ya kutoka nyumbani kwa dada yake alipokuwa akiishi.
Anasema kabla ya kuondoka kwa dada yake alimuomba
amtafutie chumba ili ajitegemea na kuanza maisha binafsi kama kijana .
Nilimwambia dada anitafutie chumba na alifanya hivyo ingawa alikuwa anahofia
kama nitaweza ,basi nikapata 'geto' langu maeneo ya Tabata Aroma na nilitakiwa
kulipa kodi ya TSh. 5,000 kwa mwezi, anasema Masanja. Anakiri wazi kuwa
changamoto katika maisha ndizo zilizochangia kumfikisha mahali alipo sasa kwani
licha ya kuwa katika hali ngumu
Hakukata tamaa bali alizidi kujituma kwa nguvu zake
zote. Anasema kuna wakati ilikuwa vigumu kuipata hata hiyo hela ya kodi kwahiyo
ilikuwa inamlazimu kurudi kwa dada yake kwa muda unapofikia wakati kulipa kodi.
Yaani hiyo TSh. 5,000 kuipata ilikuwa shughuli maana ilikuwa ikifika karibu na
mwisho wa mwezi narudi kwa dada kuzuga kidogo ili mama mwenye nyumba ajue
nimesafiri,anasema. Anasema alianza kwa kulala chini mpaka siku alipofanikiwa
kupata fedha kidogo iliyomuwezesha kununua godoro la sufi jambo ambalo
anajivunia nalo kwani aliweza kununua kwa jasho lake.
Anaongeza kuwa kamwe hawezi kumsahau marehemu Steven
Kanumba pamoja na mtu mwingine aliyemtaja aitwaye Mtitu kutokana na mchango wao
uliosaidizi kumfikisha hapo alipo sasa.
“Namshukuru sana marehemu Kanumba alikuwa anakuja
kunichukua kule Tabata tunaenda kupiga 'inshu' ambazo zilikuwa zikiniingizia
pesa kidogo iliyoniwezesha kuishi hata hivyo maisha yalikuwa magumu. Wakati
naanza maisha sikuwahi kutoa hela hata ya kununua chipsi kavu lakini siku moja
nilifanya kazi na Mtitu ambayo alinilipa laki moja sikuamini macho yangu, kwa
mara ya kwanza kununua chipsi kuku kwani nilikuwa nikitamani mlo huo
nililazimika kusaidia kumenya viazi kwa washikaji” alieleza Masanja.
Sambamba na uchekeshaji Masanja pia amejiingiza katika
shughuli za kumtukuza Mungu baaada ya kuokoa na sasa anafanya vizuri pia katika
uimbaji wa nyimbo za injili na kesho Jumapili atazindua albamu yake ya pili ya
muziki wa Injili inayoitwa Hakuna jipya chini ya jua.
(Kwa hisani ya Bongomovies.com)
0 comments:
Post a Comment