
Kituo kimoja cha redio kinachoongwa na wanawake kimeanza
kufanya kazi nchini Somali wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Redio Duniani.
Wanawake nchini Somalia, ambayo ni miongoni mwa nchi
hatari kabisa kwa waandishi wa habari, wameanzisha kituoc ha Redio Aman katika
mji mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.
Kituo hicho kinalenga kusaidia sauti ya wanawake
kusikika katika nchi ambayo ubakaji na ghasia zimetamalaki.
“Unapoanza kufanya kitu lazima ukutane na changamoto
mbalimbali. Nasi pia tunakutana nazo. Watu wanatuuliza kwa nini tunafanya hivi,
kwa sababu huko nyuma mabinti hawakuwahi kufanya kitu kama hiki,” anasema
meneja wa redio hiyo, Farhiyo Farah Aoble.
“Tumeonesha kuwa mtazamo wao sio sahihi na sasa
tumetengeneza jukwaa ambalo sauti ya wanawake wa Kisomali inaweza kusikika,”
alisema.
Badala ya kujadili kuhusu masuala ya siasa, redio hiyo
imejikita kwenye masuala yanayohusu jamii kama vile elimu, maendeleo ya jamii,
afya na masuala mengine yanayoigusa jamii.
“Ninataka kuzungumza kwa niaba ya wale walionyimwa fursa
na wale ambao sauti yao haisikiki. Tunajikita zaidi kwenye masuala ya jamii,
wanawake, huduma za afya, elimu na ujenzi wan chi,” anasema mhariri wa kituo
hicho, Aniso Abdullahi.
Watu wengi nchini Somalia huitumia redio kupata taarifa
mpya na kusikiliza vipindi mbalimbali na muziki. Kwa mujibu wa takwimu kutoka
nchini humo, mji mkuu pekee una zaidi ya vituo 28 vya redio.
Februari 13 ni Siku ya Reddio Duniani. Kauli mbiu kwa
mwaka 2014 ni “Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wanawake kupitia Redio”.
0 comments:
Post a Comment