Kwa mujibu wa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah,
Bunge la Katiba litaanza shughuli zake rasmi kesho kwa kusomwa kwa tangazo la
kuitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Siku hiyo pia kutafanyika uchaguzi wa mwenyekiti wa muda
ambaye kazi yake kubwa itakuwa ni kuandaa kanuni za Bunge Maalumu la Katiba
ambalo litakuwa na wajumbe 629.
Alisema baada ya kupatikana kwa kanuni, Ijumaa
kutafanyika uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wake kwa kuzingatia sheria ya
Mabadiliko ya Katiba iliyopitishwa mwaka jana.
Alidokeza kwa kusema pia kuwa wateuliwa, Katibu na
msaidizi wake wa Bunge hilo na kwa mujibu sheria hiyo, ataanza kazi baada ya
kuapishwa na Rais na baada ya kuapishwa naye atamwapisha mwenyekiti wa Bunge
hilo.
Baada ya mwenyekiti kuapishwa, atawalisha kiapo wajumbe
wengine wa Bunge hilo, kazi ambayo itafanyika kwa siku tatu hadi Jumatatu
asubuhi na mchana wake, Rais Kikwete atalizindua rasmi.

0 comments:
Post a Comment